GAZETI LA UCHAMBUZI MAKINI LENYE KUIHUSU NA KUIGUSA JAMII. NI GAZETI LA KILA WIKI. LITAANZA KUONEKANA MITAANI JUMANNE, MACHI 31, 2009. USIKOSE NAKALA YAKO!
Sunday, September 23, 2007
Nimekabidhi!


Nilipokuwa Sweden miezi kadhaa iliyopita nilikutana na Msweden mpenzi wa kandanda. Aliangalia picha za vijana hao wa Gangilona Kids na akaona wanahitaji msaada wa vifaa vya michezo. Kama mchezo, aliahidi angenitumia kwa posta. Juzi hapa vimefika; jezi seti mbili, mipira sita, viatu kwa wachezaji kumi na nne na simu ya mkononi ya kocha.Vyote hivyo ni kwa timu ya watoto chini ya umri wa miaka 12. Thamani ya vifaa hivyo ni karibu shilingi za Kitanzania milioni moja na nusu. Pichani ni jana mchana wakati nikikabidhi vifaa hivyo kwa kocha wa timu hiyo Rashid Zongo na nahodha Immanuel Shoo.
 
©Maggid | Date:23.9.07 | Permalink| | Send To Your Friend |


Comment: 28


  • Date: Sun Sep 23, 05:16:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    I see Mzee Mjengwa kampeni zako za ubunge ndio zimeanza tena!!

    tunahitaji watu kama wewe bungeni....

     
  • Date: Sun Sep 23, 05:17:00 PM EAT, Anonymous NDAKI

    Safi sana mwenyekiti nakupongeza kwa jitihada zako.


    Kila mmoja akiamua anaweza kutoa mchongo katika kupambana na matatizo mbalimbali .Sio kukalia kila siku semina,warsha zisizokuwa na mwisho.

    Kwa kweli umenipa changamoto kubwa sana.Ngoja na mimi nijipange nikirudi Iloganzala au Mkididili au Lenzenze au Mugoma japo niwapelekee kichochoe chochote cha maendeleo.

    Si niwe kama wale wakirudi bongo kazi blaa blaa nyiiingi na picha nyingi za kwenye minara na sanamu.


    Na sio lazima kutoa kutoa mchango wa material tu,hata kuwapatia maarifa mabayo yatawasaidia.

    Maana binafsi naamini sana kwenye ule msemo.'kumfundisha mtu mbinu ya kuvua badala ya kupatia tu samaki'.

    Hongera sana mwenyekiti.Hapo ndio kizazi kijacho cha Taifa stars.

    Nimefurahishwa na kitendo chako.Changamoto hiyo wanakijiji.Wengine mnajiita wapenzi wa soko wakati mmesimama pembeni kusubiri makosa kulaumu na ushindi kushangilia bila kutoa michango yenu.

    Hao unawaona wang'aa EUFA wameanzia ligi za michangani.Charity begins at home.

    napenda sana watu wanao wakumbuka kundi la watoto katika jamii yetu.

     
  • Date: Sun Sep 23, 05:26:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    kaka maggid,nilikuwa na subiri hii siku kwa hamu kama unakumbuka maongezi yetu ulinigusia hili swala la vifaa vya mpiga wa miguu.Huu ni uzalendo tosha kama waTanzania wote tungekuwa na uzalendo kama wa ndugu yetu Maggid tungefika mbali.
    HANGERA KAKA MAGGID MJEGWA.

    Luihamu.

     
  • Date: Sun Sep 23, 05:29:00 PM EAT, Anonymous Kidudumtu

    Well done,
    Umeonyesha njia. Keep it up!

     
  • Date: Sun Sep 23, 06:10:00 PM EAT, Anonymous MDAU bham

    Magid saafi sana umenikumbusha uwanja huo wakati wa mechi za Lugalo Sekondari na Highland sekondari miaka ya 1990

     
  • Date: Sun Sep 23, 08:11:00 PM EAT, Anonymous Mkweli

    Huu ni mfano wa kuigwa na lika mmoja wetu.

    Niliposema sema kuwa serikali haiwezi kufanya kila kitu ili kujipatia maendeleo yetu, ninaamini nilikuwa sawasawa na nitaendelea kuamini hivyo.

    Kwa yale mambo tunayoweza kuyafanya kwenye jamii zetu ili kujiletea maendeleo, tuyafanye tena ikibidi kwa haraka sana ili tupige hatua na kujikwamua hapo tulipo.

    Natoa hongera sana kwa Mdau aliyetoa vifaa hivyo kwa ajili ya jamii hitaji na pia nakupongeza Maggid kwa uratibu wako.

    May God Bless you all.

     
  • Date: Sun Sep 23, 08:47:00 PM EAT, Anonymous Born Again Pagan

    That's fantastic!

    Sasa mradi wa kuanzisha ni namna ya kujitegemea!

    Moja, ni kwa wazazi wa hao watoto...pengine wawe na shamba la kuku (chicken farm) wa kuuza nyama na mayai. Halafu watafutiwe tenda ya kulisha shuleni au migahawani.

    Mbili, kila mzazi ajitolee kuweka akiba kidogo kidogo (kadri ya makubaliano yao).

    Tatu, kila mwisho wa juma kuwe na mashindano. Kila anayetaka kuhudhuria alipishwe kidogo au watazamaji wahimizwe kutoa "donation".

    Pesa zikipatikana zinawekwa akibani ili kununulia vifaa vya michezo.

    Nne, ni kwa Halmashauri ya Wilaya kujaribu kusaidia baada ya hayo mawili kutekelezwa.

    La sivyo, hivyo vifaa vipya vikizeekea, watoto hao watarudi kwenye "square one"!

    (Sijui kama kupe matapeli nao wataingilia na kudidimisha juhudi hizo)!!!!

     
  • Date: Sun Sep 23, 08:52:00 PM EAT, Anonymous Born Again Pagan

    Kuniradhini:

    Nne, ni kwa Halmashauri ya Wilaya kujaribu kusaidia baada ya hayo mawili kutekelezwa.

    ISOMEKE:

    Nne, ni kwa Halmashauri ya Wilaya kujaribu kusaidia baada ya hayo matatu kutekelezwa.

    NA

    (Sijui kama kupe matapeli nao wataingilia na kudidimisha juhudi hizo)!!!!

    ISOMEKE:

    (Sijui kama kupe matapeli nao wataingilia na kudidimiza juhudi hizo)!!!!

     
  • Date: Sun Sep 23, 08:58:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Kwako Mkweli.
    KUAMINI na UKWELI HALISI wa jambo au Kitu fulani ni vitu viwili tofauti.Nadharia yeyote inayoanza na IMANI huwa ni mfu.Ukiamini mkeo ni mwema na hana tabia za ajabu hata kama atazaa na jirani yako utasema mtoto ni wa kwako,na utaibuka na hoja za kusema watu wana wivu na wanakuonea gele incase kama watakwambia ukweli.
    Kwa hii imani yako na serikali yako kuhusu namna ya maendeleo hatuwezi kukushawishi ukaelewa tofauti kamwe,ukizingatia hiyo ndiyo imani yako.Ila ukikua utaacha na utaelewa tofauti.
    Majita

     
  • Date: Sun Sep 23, 11:49:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    badlisha haya mashati ya batiki unaonekana mchafu hata kama ndiyo unajivuna utanzania /uafrica unaonekana mchafu tuu badilisha vaa mashati mengine au huna tukuchangie

     
  • Date: Mon Sep 24, 12:46:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Anony hapo ju sijaona mtu wa ajabu kama wewe. Huwezi kumchagulia mtu style yake ya mavazi. Ndo ninyi mnaofikiri kuvaa vizuri ni lazima uvae suti. Acha mambo ya kishamba.

     
  • Date: Mon Sep 24, 01:27:00 AM EAT, Anonymous Mlalahoi

    Mnanishangaza nyoote!
    Baada ya kumsifu aliyetoa vifaa hivyo kutoka Sweeden, nyie mnammwagia sifa Majjid. Majjid yeye si mtoaji yeye katumia vifaa posta ( kama alivyofafanua juu), yeye alichkifanya ni kukabidhi mzigo kwa wausika!

    Ndo nyie wale kiongozi anaenda Ulaya, anapata misaada, nyie badala ya kuwasitu wakatwa kodi nchi husika mnaanza kumwaga sifa kwa mara Kikwete, Mkapa!

    Duh kazi ipo kwa watanzania~

    Mdau wa Sweeden nakushukuru kwa hilo, majjid na wewe asante kwa kukabidhi!

     
  • Date: Mon Sep 24, 02:26:00 AM EAT, Anonymous NDAKI

    Mlalahoi,ngoja nikujibu sababu za kumpongeza Mwenyekiti(Maggid)

    Hapa hatuangalii matoke(kitendo cha kukabidhi).
    Binafsi nimetoa pongeza kutokana na jitihada alizo onyesha tangu awali katika kuwatangaza hao watoto na hadi kufikia hatua ya kupata mtu aliyekuwa tayari kuwasaidia.


    Pili, Nampongeza kwa kuwa mwaminifu na kufikisha kunakohusika huo msaada.

    Tofauti za baadhi ya viongozi wetu,hata kama tutapewa mkopo wa masharti magumu au msaada.Hata hicho tunachokopeshwa hakitufikii chote,ndio kinaishia kwenye matumbo yao.

    Kwani unafikiri mwenyekiti naye angekuwa FISADI si angeamua hivyo vifaa aingie kariakoo faster awauzie wenye maduka kwa jumla.

    Lazima twende mbele na kurudi nyuma.Mwenyekiti anastahili pongezi.

    Pia mlalahoi,naungana na wewe pia inatupasa pia kumshukuru na huyo mfadhili aliyekubali kutoa huo msaada.

    Ni hayo tu kwa leo

     
  • Date: Mon Sep 24, 02:46:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Ndaki, maneno yako yote ni sahihi.
    Nakuunga mkono kama wanakijiji wengine walivyokuunga. Misaada mingapi inatolewa kwa ajili ya kusaidia maendeleo yetu inayoishia kujenga majumba binafsi, kuoa mke mdogo n.k. Wengine wanadiriki hata kutia ndani misaada ya watoto yatima, misaada ya kidini, misaada ya kujenga zahanati, madaraja na mingineyo. HONGERA MWENYEKITI, KAZI NZURI!

     
  • Date: Mon Sep 24, 03:19:00 AM EAT, Anonymous NDAKI

    # Jina: Mjengwa
    # Nipo: Afghanistan
    # Tel no: + 255 754 678 252
    # E-mail: maggid@hotmail.com

    Samahani mwenyekiti nimestuka kidogo na taharifa yako hapo juu.Naona anwani yako chini ya picha yako inaonyesha NIPO:Afghanistan.

    Nafikiri unaweza kunisaia maana naona huko uliko ni mbali na hapa bongo.Uliondoka baada ya kukabidhi zawadi?Au nini malengo ya kuandika uko Afghanistan?Je huko unaendelea kustumia number hiyo ya vodacom kama inavyoonyesha?


    Nitashukuru ukinipatia ufafanuzi huo.

     
  • Date: Mon Sep 24, 03:47:00 AM EAT, Anonymous NDAKI

    Kumradhi huo mstari

    "Je huko unaendelea **kustumia** number hiyo ya vodacom kama inavyoonyesha? "

    naomba usomeke hivi:
    Je huko unaendelea **kutumia** number hiyo ya vodacom kama inavyoonyesha?

    Poleni kwa usumbufu

     
  • Date: Mon Sep 24, 04:35:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    kampeni za ubunge hizo zimeanza mr mjengwa,tunahitaji vijana kama wewe bungeni.

     
  • Date: Mon Sep 24, 07:25:00 PM EAT, Anonymous Mdau wa Ireland

    Majjid, is a good man, and he has shown that today.

    Nakupongeza sana mkuu, umeonyesha umahiri wako katika hili, Personally I believe you are a great guy, sincere and a good model for the young people and adults a like.

    Samahanini sana kwa kuchanganya lugha.

    Mdau wako wa Ireland. Will always keep visiting.

     
  • Date: Mon Sep 24, 07:38:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Kumsifu Mheshimiwa Mjengwa katika safu hii ni kitu cha maana sana. Hasifiwi kwa maana ya kutoa vifaa bali anasifiwa kwa maana ya kuwa mwaminifu na msemaji wa wanyonge. Hakuweza kulifumbia macho suala hili bali alilifanyia kazi kwani aliguswa kwa undani zaidi. Kama asingelikuwa na nia nzuri na timu hii angeamua kukaa kimya, na kama vifaa vingekuja basi angefanya lolote atakalo ikiwa ni pamoja na kuviuza vifaa na kukaa kimya nani angejua. Je ni wangapi wamekuwa wakitumia vitu vya wenye kuhitaji kwa ajili ya manufaa yao wenyewe. Ni viongozi wangapi wamekuwa wakitafuna misaada ya wanyonge na nini kimefanyika kwao. Ndugu yangu Mjengwa umekuwa mwaminifu kwa madogo hakika utaaminiwa kwa makubwa. Mwenyezi Mungua akubariki sana na akuongezee mara utakavyo.

     
  • Date: Tue Sep 25, 08:54:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    1:- Mlala hoi kweli we ni mlalahoi maana umeongea pumba za ajabu.

    2:- Ndaki unaboa sasa we kila siku unaakosea wewe tuuuuu, tumechoka kuona jina lako likitokea zaidi ya mara tatu kwenye comments za picha moja, jirekebishe maana unaboa sasa.

    3:- Mkweli sina wasi wasi na majibu uliyopewa maana huyo jamaa hapo amekujibu vizuri sana na nampa pongezi kwa majibu aliyokupatia.

    4:- Hongera sana Mr Mjengwa kwa kweli huu ni mfano wa kuigwa maana kwa watu wengine kama MLALAHOI huo msaada usingewafikia walengwa.

     
  • Date: Tue Sep 25, 12:02:00 PM EAT, Anonymous Mlalahoi

    Itatuchukua miaka nenda rudi watanzania kuacha kujikomba kwa watu awe kiongozi au nani ilimradi mtu ana kitu fulani...

    Baada ya kutoa mada yangu mwanzo kati ya comment 20 zilizotolewa bado ni mtu mmoja tu aliyemsifia mtoa vifaa kutoka Sweeden. Mdau wa Sweeden imemgharimu si chini ya million 1.5 kama alivyosema mwenyekiti Majjid, lakini hakuna anayeliona hilo...

    Wote mnakuja na propaganda za kumshambulia Mlalahoi!

    Beauty of knowledge bado iko mbali ya upeo wa macho yetu, anyway tutafika tu...hata Roma haikujengwa kwa siku moja! Lakini kwa mwendo huu mh! ninamashaka na kufika huko...

     
  • Date: Tue Sep 25, 01:07:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Kuomba kitu hadi kupata ni kazi kubwa si ndogo.Maombi mengi siku hizi ya ufadhili wa chochote hutupiliwa mbali na wafadhili.Si rahisi kuomba na ukafanikiwa kupewa.

    Mjengwa ana haki ya kupongezwa kwa kuomba na kupewa.Kama Mlalahoi unadhani ni kazi rahisi kuomba ufadhili na kupewa jaribu na wewe ili ukipata tukupongeze.

     
  • Date: Tue Sep 25, 04:34:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    always mpuuzi mwenye wivu na mafanikio ya mtu fulani hutoa comments za kukashifu maendeleo ya huyo mtu...

    Na hili tunaliona kwa huyu bwana anayejiita MLALAHOI. Ni upuuzi tu hakuna hoja za msingi, Yes ni upuuzi na comments zako ni zanye chuki na fitina Yes chuki na fitina.

    Jiulize mlala hoi, bila mjengwa kuomba huo msaada leo hii hao watoto wangekuwa na hivyo vitu walivyovipata? Ni Mjengwa aliyetumia muda wake na kukaa chini na kupresent maombi mpaka mfadhili amekubali kumpatia vifaa hivyo vyote, na ni wajibu wetu sisi kumpongeza mjengwa maana huyo msweeden unayemsema alishapewa shukrani zake na Mjengwa ambaye ametuwakilisha sote hata wewe mlalahoi.

    Hatukulazimishi kumpa pongezi bwana Mjengwa ila hapa tumetumia haki yetu kikatiba kwa kutoa pongezi kwa bwana Mjengwa na si kukashifu.

    Ninachokushauri we mtafute huyo msweeden kwa muda wako then mpe pongezi zako mwambie kuwa unampongeza kwa sababu amempatia mjengwa vifaa vya michezo.

     
  • Date: Tue Sep 25, 09:17:00 PM EAT, Anonymous Mlalahoi

    Narudia tena wanakijiji,
    Itatuchukua muda mrefu watanzania kaucha kasumba ya kukumbatia ulafi, fitina, ugeugeu, kulamba watu viatu n.k

    Hivi kweli inawachukua hata sekunde ngapi kuandika mstari mmoja wa kumpogneza mfadhili? Inawachukua si chini ya dakika 5 kuniandama na kuendelea kuendekeza uwozo wa kumkumbatia mtu kwa kuandika mistari mirefu, lakini inawachukua siku, mwezi, pengine mwaka kuandika sentensi ya shukrani kwa mfadhili! shame on you all!!!

    Nitaendelea kurekebisha pale tunapokwenda mlama, no matter what! who cares! Baba IC upo hapo?

     
  • Date: Wed Sep 26, 08:52:00 PM EAT, Anonymous Mkweli

    Kamwe sitabishana na mjinga kwani hakuna mtu atakayeelewa nani ni mjinga miongoni mwetu.

     
  • Date: Thu Sep 27, 12:57:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Wewe Mkweli,
    Ungekaa kimya basi kama wewe si mjinga.Hiyo kujibu tu hoja wakati unasema kuwa "kamwe hutabishana na mjinga" wewe umeonekana ni taahira

     
  • Date: Thu Sep 27, 06:02:00 AM EAT, Anonymous Mlalahoi

    Duh sijasema mimi, upo hapo Mkweli? tayari umejibiwa ahaha!

     
  • Date: Thu Sep 27, 09:34:00 PM EAT, Anonymous Mkweli

    Kamwe sitabishana na mjinga kwani hakuna mtu atakayeelewa nani ni mjinga miongoni mwetu.

     
   
 
Copyright 2006 © MAGGID MJENGWA. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu