GAZETI LA UCHAMBUZI MAKINI LENYE KUIHUSU NA KUIGUSA JAMII. NI GAZETI LA KILA WIKI. LITAANZA KUONEKANA MITAANI JUMANNE, MACHI 31, 2009. USIKOSE NAKALA YAKO!
Tuesday, August 28, 2007
Baraka Au Laana?

Kuna mwanakijiji mwenzetu aliyefikiri, kuwa Iringa "IMEBARIKIWA" kwa mawe. Lakini, mlima huo na mingine ya hapa Iringa ilifunikwa na misitu kabla. Kinachoonekana hapo n i uharibifu wa mazingira. Miti yote imekatwa. Kuna vijana wa Iringa wanaokumbuka, kuwa hadi mwaka 1977, waliweza kupanda milima hiyo iliyokuwa na miti mingi. Walikwenda huko na kuwinda ngedere wakiwa na mbwa wao. Binafsi nakumbuka utotoni. Miaka ile ya mwanzoni mwa 70's nikiwa na baba yangu tulisafiri kwa basi la KAMATA toka Igawa Mbeya hadi Iringa. Hapo tulikaa siku kadhaa kwa ndugu yetu mmoja aliyeitwa Merere. Ndugu huyu aliishi Gangilonga, ilijulikana pia kama "Uzunguni". Naikumbuka Iringa iliyokuwa na miti mingi. Mawe hayo ya mlimani sikumbuki kama niliyaona. Nakumbuka Gangilonga yenyewe ilikuwa imefunikwa na miti mingi.
Nilipofika tena Iringa miaka ya 90 nikamwuliza mwenyeji wangu nikikumbuka Gangilonga ya utotoni; " Hivi Gangilonga ni wapi ? Niliuliza. " Hapa ulipo ndio Gangilonga!" Alinijibu. Naam. Tunakaribisha mawazo kutoka kwenu, juu ya namna gani tunaweza "kuikijanisha" tena Iringa na hatimaye kuyafunika tena mawe hayo yanayoonekana.
 
©Maggid | Date:28.8.07 | Permalink| | Send To Your Friend |


Comment: 46


  • Date: Tue Aug 28, 10:23:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Mkataba wa Buzwagi ulisainiwa nje haraka ili kukwepa gharama

    Habari Zinazoshabihiana
    � Udurusu mikataba ya madini wakamilika 15.08.2007 [Soma]
    � Suala la rada danadana tupu 08.02.2007 [Soma]
    � Kikwete asifia mradi wa Buzwagi 24.08.2007 [Soma]

    *Barrick yasema majadiliano yalichukua muda mrefu
    *Yasema kisheria mkataba unaweza kusainiwa popote
    *Yaeleza jinsi uchumi wa nchi utakavyokua kwa kasi

    Na Said Mwishehe

    KAMPUNI ya uchimbaji Madini ya Barrick Gold Tanzania imesema mkataba wa mgodi wa Buzwagi uliharakishwa kusainiwa Uingereza ili kuepuka upandaji gharama za uendeshaji.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Barrick Gold Tanzania, Bw. Deo Mwanyika, kutokana na majadiliano juu ya kusainiwa kwa mkataba huo kuchukua muda mrefu, Barrick iliiomba Wizara ya Nishati na Madini kuharakisha uamuzi wake kwa vile ucheleweshwaji wa utiwaji saini ulikuwa ukiuathiri vibaya.

    "Tuliona ni vema tukaharakisha utiaji saini wa mkataba huo baada ya kuona kwamba kama tutachelewa kuna hatari za kuathirika kwa mradi wenyewe kutokana na kupanda kwa gharama za vifaa kila kukicha. Kwa mfano kati ya Juni mwaka jana na Januari mwaka huu, gharama za mradi ziliongezeka kwa kiasi cha dola milioni 20 za Marekani," alisema.

    Kwa upande wa Barrick alisema kulikuwa na ulazima wa kuharakishwa utiaji saini huo kabla ya mwisho wa mwaka huu, ili makao makuu ya kampuni hiyo yaweze kuweka mgodi wa Buzwagi katika mpango wa makadirio ya mwaka.

    Bw. Mwanyika alisema kutokana majadiliano yaliyofikiwa kati yao na Wizara ya Nishati na Madini, waliarifiwa kuwa mkataba wa Buzwagi ungekuwa umesainiwa ifikapo Februari 16 mwaka huu.

    "Barrick tuliambiwa kwamba vibali vyote kutoka vyombo husika vya Serikali vilikuwa vimepatikana. Kutokana na hali hiyo waliendelea kukamilisha taratibu za kusaini mkataba Februari 16 mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuandaa maofisa wake walioidhinishwa kusaini mkataba huo na nyaraka zinazoendana na mamlaka hizo," alisema Bw. Mwanyika.

    Hata hivyo, alisema kwa bahati mbaya, ilipofika Februari 15 mwaka huu, wakaambiwa kwamba mkataba huo usingeweza kusainiwa kutokana na Waziri wa Nishati na Madini kuwa katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete katika nchi za Ulaya.

    "Kutokana na kuona kwamba kuna hatari ya kutosaini mkataba huo wakati muda unazidi kwenda, uongozi wa Barrick uliwasiliana na Wizara na kupendekeza kwamba isingekuwa vema kuahirisha utiaji saini mkataba huo, kwa vile taratibu zote za maandalizi zilishakamilika," alisema Bw. Mwanyika.

    Alisema baada ya kutoa ombi hilo, ndipo walipoarifiwa na Wizara kwamba Bw. Karamagi angepatikana London, hivyo ujumbe wa Barrick uliondoka Tanzania na kwenda Uingereza ambapo mkataba ulisainiwa Februari 17 mwaka huu katika Hoteli ya Churchil ambapo mbali na maofisa wengine wa Wizara ya Nishati kuwapo, pia Balozi wa Tanzania nchini London, Bibi Mwanaidi Maajar naye alikuwapo.

    "Ni kweli tulisaini hotelini na hilo si kosa, kwani mkataba unaweza kusainiwa mahala popote pale, ilimradi uzingatie sheria na taratibu. Kuhusu nani alichukua mhuri na nyara nyingine za Serikali, hadi Uingereza hatujui, ila inawezekana ni maofisa waliokuwa Tanzania ambao tulikuwa tukijadiliana nao juu ya suala hilo nchini na baadhi yao tulikuwa nao wakati wa utiaji saini, hivyo inawezekana ndio waliokwenda na nyaraka hizo za Serikali," alisema.

    Hata hivyo alisema Barrick haina ofisi wala kampuni Uingereza na wao pia walikuwa wageni ambao walikwenda huko kwa jukumu la kuhakikisha mkataba unasainiwa kama ilivyokuwa imepangwa na kukubalina na Serikali. Lakini ni vema mambo mengine muwaulize maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini," alisema.

    Akieleza zaidi juu ya mgodi wa Buzwagi, Bw. Mwanyika alisema pamoja na kusaini mkataba, bado kwa sasa mgodi huo hauna faida kutokana na kwamba hauna dhahabu ya kutosha, ambayo inalingana na gharama zitakazotumika kujenga mgodi huo.

    Alisema mradi wa machimbo ya Buzwagi ni mgodi mdogo unaohitaji uwekezaji mkubwa wa dola milioni 400.

    "Mradi wa Buzwagi ni mdogo, kwa sababu pamoja na kutumia dola milioni 400 ili kuuchimba, utazalisha wakia milioni 2.4 ikilinganishwa na mgodi wa Bulyanhulu ambao ulitumia dola milioni 280 kutoa wakia milioni 10 za dhahabu," alisema Bw. Mwanyika.

    Alisema kutokana na kukosekana kwa dhahabu ya kutosha katika mgodi huo, hakuna kampuni ya uchimbaji duniani ambayo ingekubali kusaini mkataba wa uchimbaji madini ambao utaleta faida ya sh. bilioni 800 kutokana na makato ya kodi mbalimbali kwa kipindi cha miaka 10.

    Alisema mbali na Serikali kupata kiasi hicho cha fedha, pia wanakijiji wa Mwima ambao ndio wako katika eneo la mgodi wa Buzwagi, wamelipwa fidia sh. milioni 78 mbali na sh. milioni 60 zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wana kijiji.

    Vilevile wakati wa ujenzi wa mgodi huo, uchumi wa Tanzania utaongezeka, kwani wakati wa ujenzi kiasi cha sh. bilioni 450 zitapatikana na wakati wa uzalishaji, sh. trilioni 1.3 zitapatikana katika kipindi chote.

    "Kusainiwa kwa mgodi wa Buzwagi, nchi itapiga hatua kiuchumi, kwani wananchi watafaidika na mgodi huo kutokana na ajira zitakazopatikana, lakini pia ni kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanaboreshwa hasa walioko eneo husika," alisema Bw. Mwanyika.

    Alisema ajira mpya zaidi ya 900 zitatokana na uwekezaji huo katika kipindi cyha ujenzi na kuingiza jumla ya sh. bilioni 75 kama mishahara.

    "Vile vile kutakuwapo na ajira nyingine 700 zitakazoingiza jumla ya sh. bilioni 130 wakati wa uendeshaji wa mgodi," alisema Bw. Mwanyika.

    Mgodi wa Buzwagi umeingia katika duru za habari baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kuwasilisha hoja bungeni akidai kuwa kitendo cha kusaini mkataba wa mgodi huo nje ya nchi kilikuwa na dosari.

    Bw. Kabwe kutokana na hoja yake, alitaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mazingira ya mkataba huo akidai kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Karamagi, alikuwa amelidanganya Bunge. Hata hivyo mambo yalimgeuka na kujikuta akisimamishwa kazi hadi Januari mwakani

     
  • Date: Tue Aug 28, 10:23:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Napendekeza Wanafunzi wote kuanzia msingi hadi vyuo vyote vilivyopo hapo Iringa mjini na wakazi wote wa Iringa Mjini kila moja apewe miche ya miti 10 tu aipande kwenye hiyo milima.

    Kama miti hamna ombeni Wizara ya mali asili,wizara ya kilimo au serikalini ya mkoa wawape miche ya miti kama wakikataa kuwapa hiyo miche Mjengwa Tuambie kwenye hii blogu tutafute watu watakaotoa hiyo miche ya miti ya kupanda ila serikali ya mkoa itabidi yote ijiuzulu kama watashindwa kujua miche ya miti watapata wapi kiasi cha kufanya wanablogu waitafute.

    Nashauri Iteuliwe siku maalumu ambapo wanafunzi watapanda hiyo miche 10 ya miti kila mmoja kwenye hiyo milima halafu ifuate siku ingine ya wakazi wote wa huo mji kuipanda.

    koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Tue Aug 28, 05:06:00 PM EAT, Anonymous Miriam

    Mkubwa wa mkoa yuko wapi? hili lingekuwa swai zuri kwa watu wanaogombania viti Iringa

     
  • Date: Tue Aug 28, 05:54:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Koloboi, ukizingatia Iringa inapata mvua ya kutosha karibu kila mwaka, wazo lako ni zuri sana.

    Ushauri wangu kwa suala hili la upandaji miti hapo Iringa.

    Ninahisi ni rahisi sana kupanda miti na ikue vizuri sana.

    Iwapo wananchi watahamasishwa kupanda hiyo miti na kuonesha kusita, watumike wafungwa.

    Nadhani hawa (wafungwa) ni nguvu kazi nzuri sana ambayo ikitumika mbali ya kushiriki kufufua mazingira yaliyokufa, watakuwa wanajifunza jinsi ya kutunza mazingira na wakitoka huko usishangae baadhi yao wakawa wanamazingira wazuri sana.

    Hawa watu wanatakiwa watunzwe na wafanye yale ambayo ni manufaa kwao nakwa jamii.

    5 5 5

     
  • Date: Tue Aug 28, 06:02:00 PM EAT, Anonymous NDAKI

    WANAKIJIJI NDIO MAANA NIMEOMBA KWANZA MAGGID ATUSAIDIE PICHA ZA VYUO VYA TUMAINI NA MKWAWA.

    HII ITATUSAIDIA KUJUA HAWA WASOMI WALIOPO HAPO KAMA WAMEFANIKIWA KUTUNZA KWANZA MAZINGIRA YA KWAO.

    KAMA JIBU NI NDIO BASI WATUAMBIA HIVI WAMERIDHIKA KWELI NA HALI YA MAJIRANI WANAOWAZUNGUKA?
    WAKUMBUKE MAZINGIRA NI UHAI. SIO SEMINA NA MAWEKSHOPU YAO KUTUMBUA FEDHA ZA MAZINGIRA TU.
    HIVI MKOA HAUNA HATA AFISA MISITU?KAMA YUPO KAZI YAKE NINI?AU NI KUUZA MBAO ZA MITI MICHACHE ILIYOSALI?ANASHINDWA HATA KUBUNI NINI KIFANYIKE?ENE WEI TUTAFIKA TU

     
  • Date: Tue Aug 28, 07:19:00 PM EAT, Anonymous Mti

    Wajihadhari na landslides! mawe yanajiandaa kuporomoka, kama mabomu!

     
  • Date: Tue Aug 28, 08:36:00 PM EAT, Anonymous Makafoo

    Mwenyekiti na wanakijiji,
    Hili ni suala nyeti kwelikweli lakini approach zinazopendekezwa hapa ni za zimamoto kama kawaida ya Watanzania.
    Kuamka siku moja na kwenda kupanda miti kwenye milima hiyo ni suala moja na kuhakikisha miti hiyo inakua ni suala jingine. Nani atailinda miti hiyo dhidi ya mbuzi na ng'ombe wanaochungiwa humo milimani? Nani atatoa maji Ruaha na kupandisha nayo huko mlimani kwenda kumwagilia? Siyo kweli Iringa inapata mvua karibu mwaka mzima, hiyo ilikuwa Iringa ya miaka ya 70 na mwanzoni mwa 80 kabla ya uharibifu huu wa mazingira. Kwa sasa Iringa ni moja ya sehemu kame Tanzania.
    Hebu tujikumbushe miti mingi iliyopandwa na watawala wetu kwa mbwembwe siku za mazingira, sijui siku ya afya n.k Miaka michache iliyopita Meghji alipanda mti pale chuo Kikuu katika kilele cha maadhimisho fulani. Huo mti leo haupo na hata yeye sidhani kama ana kumbuka kama aliwahi kupanda mti.
    Milima kama hii inafaa imilikishwe kwa watu wenye kuona mbali ambao wanaweza kupanda na kutunza miti itakayopandwa. Wtz wengi hatujui faida ya miti, kwa hiyo hatuwezi kuwekeza kwenye mradi unaohitaji miaka 10 hadi 20 kulipa.

     
  • Date: Tue Aug 28, 08:49:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Kuna "methodology" mpya siku hizi inatumika kutunza mazingira. Mambo ya wanafunzi na wafungwa siyo ya kutegemea sana maana miti inachukua miaka kumi hadi hamsini kuwa msitu. Mbinu hii ni ya "kushirikisha" wananchi.

    Kwa kifupi, wanasiasa wanachukulia hii concept kama ni rahisi lakini siyo. Watu wa Iringa wanatakiwa wa "own" hiyo milima. Ofisi ya misitu ishirikiane na ofisi ya maendeleo ya jamii ku-enforce hilo.

    Vyuo vikuu navyo vipewe "ownership" ya baadhi ya hizo hills. Wazungu wanasema "the magic of ownership turns sands into gold" Cha wote hakina mwenyewe na cha umma hakiumi!!

    Mambo ya nationalization ndiyo yaliondoa link kati ya watu na mazingira yao hivyo watu wanafikiri milima na mabonde ni mali ya serikali.

    Kuhusu ushirikishwaji wahadhiri wa hivyo vyuo wanaweza wakaombwa ushauri. Nina uhakika ni vigumu serikali kuimba huu wimbo. Ni wimbo mpya kwa watendaji wa serikali siyo tu ya Tanzania bali nchi nyingi za kiafrika zenye harufu au zilizo wahi kupitia ujamaa. Na hamna wa kumlaumu, siyo afisa misitu wala mkuu wa mkoa. Ni policy ya nchi ilikuwa hivyo. Kila kitu kilionekana cha serikali.

    Kwa kuwa wanachi wa hapo Iringa hawafaidiki kiuchumi wala kijamii na hiyo milima (kwa mfano hawapati kuni, hawavuni asali) ku-win acceptance yao inahitaji high degree of understanding of social cultural issues. Serikali za vijiji zipewe "milki" ya vijisehemu vya milima na kila mwaka kutolewe zawadi ya kijiji kipi kina boresha mazingira kuliko kijiji kingine. Kinyume na hapo ma NGO na ma NGO yatakuja, kila kiongozi atakuja na kulipwa mishahara, kampeni za kitaifa za kupanda miti zitafanyika but I promise you, NOTHING will change!!

    Wenzetu wa nchi nyingine wako mbali sana katika hii falsafa ya ushirikishwaji. Nchini Mali hata miti ya asili (mti mmoja mmoja) ime "milikishwa" kwa wananchi wa vijiji husika na haiwezekani serikali ikatoa kibali eti cha kuvuna magogo bila wanachi kushirikishwa. Nchini kwetu siyo tu kwamba serikali za vijiji hazipo kwenye katiba ya nchi bali hata serikali za mitaa yaani Local Governments hazina uhuru wa kutosha wala maamuzi ya matumizi ya rasilimali. The central government owns every thing! Wanakijiji ni mere occupants na ardhi yote iko chini ya rais kama trustee. We need to change some of these colonial things.

    Ninaweza kabisa kufanya hypothesis kuwa bila kuwa-win wanachi wa Iringa wakasahau mambo ya villagilization, serikali kumiliki kila kitu na kadhalika hakuna mtu atatunza milima mitupu. Falsafa hii inaweza isifanye kazi Longuza au Arumeru kwani watu bado wanaiona faida ya misitu. Hapo Iringa mjini wanaona faida gani?

    Nimalizie: change an individual, then a society and then the environment. The otherway round will NEVER work! Adui wa mazingira ni mtu.

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Tue Aug 28, 09:04:00 PM EAT, Anonymous NDAKI

    daima sisi sisi wanakijiji uwa tunapiga makofi point nzito kama hiyo ikitolewa.hongera sana.
    Ombi langu,nakuomba kaka Maggid hayo mawazo mazuri ya mh.Munge uyabebe kama yalivyo yawakilishe kwa afisa misitu nakala na RC,DC,Tumaini na Mkwawa.
    Inawezekana.TUTAFIKA TU!

     
  • Date: Tue Aug 28, 10:41:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Watanzania inabidi tujifunze kutoa practical solutions zinazoweza tatua tatizo badala ya classroom arguments ambazo hazitoi ufumbuzi haraka wa tatizo bali zinaongeza muda wa kujadili tatizo.

    Mambo yafuatayo inabidi yafanyike kwa mpangilio ufuatao .

    1.Huo mlima inabidi ufunikwe na miti badala ya upara.Hivyo miti ipandwe iwe na wanafunzi,wanavijiji, wafungwa n.k si issue. Issue ya kwanza panda miti.

    2.Ukishapanda miti shughulikia tatizo la nani amilikishwe hiyo miti iliyopandwa kama ni kijiji,chuo au nani ili ailinde na kuitunza. Zungumzia hilo baada ya kupanda.Ukitaka ulizungumzie kabla ya kupanda kwa watanzania nijuavyo itachukua karne kabla ya kupanda hiyo miti.Watanzania wanapenda sana vikao.Na vikao hivyo vikianza watadai posho na hela za usafiri wa kwenda kwenye vikao vya kujadili .Itachukua miaka kupanda hiyo miti.

    3.Miti hiyo ipandwe wakati wa mvua za masika.Wala hakuna haja ya kufuata maji mtoni kama mmoja alivyoshauri ili aonyeshe kuwa huo mradi huo ni mgumu kutekelezeka.Kilimanjaro na Mbeya wamepanda mamilioni ya miti wakati wa mvua za masika hadi leo ipo na hakuna aliyechota maji kwenda kuimwagilia.Watu wengi wa Mbeya na Kilimanjaro hutumia kuni kutoka miti waliyojipandia wenyewe karibu na nyumba zao huoni wengi wakienda kukata miti milimani kama hao wakazi wa Iringa.

    Milima kama hiyo kuijaza miti inataka MASS CAMPAIN ya zimamoto kama kampeni za kitaifa. Ukitumia watu wachache kujaribu kujaza miti milima hiyo kutachukua miaka mingi.Ndiyo maana inatakiwa kampeni kubwa ambayo una uhakika ndani ya siku Saba wakati wa mvua za masika milima hiyo yote iwe umejaa miti.Kufikia lengo kama hilo unahitaji mass campain

    Wakati wa masika mwaka huu ndio muafaka wa kupanda miti kwenye hiyo milima.Watu wa Iringa acheni uvivu.Miti ya Ulanzi (MIANZI) mbona huwa mnaipanda kwa wingi bila kilimo cha umwagiliaji?Zikianza mvua za masika miti ipandwe.Acheni porojo watu wa Iringa Mjini.

    4.Iringa igeni Kilimanjaro na Mbeya ambako vijijini kwa mfano wilaya ya Rungwe karibu kila mtu ana miti yake kwa ajili ya kuni za kupikia aliyopanda mwenyewe karibu na nyumba yake au kwenye shamba lake na wamepiga marufuku mtu kukata miti kwenye milima na kwenye eneo lisilo shamba lake au eneo lake.Kilimanjaro na kule Rungwe Mbeya si rahisi ukutane na mtu anatoka kukata kuni milimani.Wengi hukata kuni kwa kuangusha mitiulaya waliyopanda karibu na nyumba zao.

    Wasomi ni wakati wa kutoa action practical oriended advice zinazotoa results haraka badala ya kutoa mawazo yanayongeza tu urasimu kwenye utekelezaji.

    Mjengwa niko mbali ningekuwa karibu ningefanya kama Reginald Mengi ambaye aliona badala ya kusubiri wasomi,wabunge na wanasiasa wajadili upandaji miti kilimanjaro akaona aanze kupanda miti.Akapanda mamilioni.

    Mjengwa mimi nafikiri Iringa inahitaji sana wapanda miti na na haihitaji kabisa kwa sasa wataalamu wasomi wa kujadili na kuandika makala ndefu za kina zinazozungumzia kuhusu upandaji miti kwa undani na kwa kitaalamu.

    Na pia sidhani Iringa inahitaji wabunge na vikao vyao vinavyoweza zungumzia kwa uchungu uharibifu wa mazingira.Iringa inahitaji miti si maneno ya wabunge wala makala za makaratasi za kitaalamu.

    Mjengwa badala ya kupeleka mawazo kwa RC,Mbunge,Afisa misitu,na hao wanavyuo ukienda naomba kawambie winuke waende wakapande miti.

    Ukimwona RC,DC,Mbunge,Afisa Misitu na hao wasomi waambie wainuke haraka wakapande miti kwenye hiyo milima.Usikubali mjadala nao.Mhimize hasa RC na DC wawahi haraka kupanda miti waache peni na makaratasi waende kupanda miti haraka.

    Ukimwona Afisa misitu mwambie nampa mwaka mmoja vinginevyo nitampeleka mahakamani kumshtaki kwa kula hela za walipa kodi kwa utapeli, sababu anajiita afisa misitu wakati misitu hamna kuna mawe tu kwenye hiyo milima.Ni heri angejiita afisa mawe na si misitu.Lakini kwa kuwa anajiita Afisa misitu atakuja kunitambua baada ya mwaka kama hiyo milima itakuwa haina misitu.Kama hanijui aningojee baada ya mwaka.Mjengwa file hii mesage yangu ili tarehe kama hii mwakani kama hiyo miti itakuwa haijapandwa uone huo moto utakaowaka kama unadhani natania na uwe na reference.

    koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Tue Aug 28, 11:09:00 PM EAT, Anonymous NDAKI

    natoa wazo wanakijiji wenzangu.
    Mnaonaje hiyo huyu afisa misitu wa hapo IRINGA kama alivyosema Koloboi aitwa AFISA MAWE au afisa JANGWA?

    maani ni sawa ni kuwa na afisa UVUVI jangwani pakame.Misitu iko wapi?ya kuhesabu.
    ENE WEI TUTAFIKA TU.

     
  • Date: Wed Aug 29, 12:29:00 AM EAT, Anonymous ANALYST

    Koloboi leo sikubaliani na wewe hata kidogo. Kumbuka kila kiongozi anayepangwa Iringa anapewa ultimatum kuboresha mazingira. Such kind of zimamoto and ambush kwamba baada ya mwaka mmoja unamshitaki mtu, WILL NEVER WORK. Nasisitiza this is a social cultural issue na niko tayari kuandika hata kurasa ishirini.

    Pia utofautishe uoteshaji wa miti mijini unaofanywa na Mengi kanda ya kaskazini na regenarating nature in a semi desert environment like Iringa away from peoples settlement.

    People should be taught and mobilised at the grassroots and not to organise compaigns watu wapande miti ili wapigwe picha na waandishi wa magazeti. Planting a tree is one thing, nursing such trees to become a forest is quit another.

    Kama nilivyosema awali it is the society which changes the environment and not the other way round. Kupanda miti hata millioni ishirini hakubadili attitude ya wananchi. Wanaweza wakaikatilia mbali kabla hata haijakuwa kama walivyofanya enzi za waingereza baadhi za makabila kuchemsha mbegu za karanga za waingereza.

    Society is a complex institution. Almost every kind of problem we are trying to solve through volumes of research reports and even laboratories can easily be solved if we sit down with the community and use their very own solutions. Hakuna fani yeyote iwe misitu, mali asili, biashara au nini siku hizi hawafundishi aspects za community empowerment. Ukikuta hawagusii mambo ya jamii ujue hiyo silabus ni ya enzi za mkoloni. Our knowledge fountain and the power to do or refrain from doing rests with the common man in the village. Kinyume na hapo ni ukoloni au ukoloni mambo leo au vyote viwili!

    Wenzetu wa nchi zingine wako mbali sana. Mwananchi siyo tu ni bosi wa wanasiasa bali pia ni profesa wa wataalamu. It is high time we go back to square one na siyo kutishia viongozi nao wakawatishie wananchi. Mkuu wa mkoa akisikia hivyo atatuma mgambo wakalazimishe watu kupanda miti, and what do you think will change??

    Magid ukiamua kufanyia kazi hili tuwasiliane kwa mjadala zaidi. It has worked in many parts of Africa why not Iringa?????

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Wed Aug 29, 08:19:00 AM EAT, Blogger Mjengwa

    Wanakijiji,
    Asanteni sana kwa michango yenu yenye kujenga. Naahidi kuyachapisha mawazo yenu haya na kuyafikisha kwa wahusika juma lijalo. Nitarudi hapa na majibu yao.

     
  • Date: Wed Aug 29, 09:39:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Mjengwa samahani kwa kurudi tena nimalizie kujibu Mheshimiwa Blogger mzuri Analyistmunge.

    Analyistmunge ni haki yako kabisa kutofautiana nami.Nami naheshimu haki yako hiyo na mawazo yako.

    Lakini Analyist naona unauonea ukoloni kwa kuutazama kwa jicho baya tu.

    Napenda kukujibu kuwa ukoloni Tanzania hasa wa kijerumani na kireno umefanya vizuri sana kwenye baadhi ya maeneo.

    Mfano mahindi yaliletwa na wakoloni wa kireno wakalazimisha watu kulima kwa nguvu sababu halikuwa zao waliolizoea . Hadi leo ni mahindi ni chakula kikuu cha makabila ya Tanzania.Jamii zilikuwa zinalia kupinga kulazimishwa kulima mwanzoni bila kushirikishwa washiriki kwa hiari lakini baadaye kila jamii ina hamu na mahindi na inalima bila kulazimishwa..

    Pamba,kahawa na Chai zililetwa na wakoloni wakalazimisha wananchi kulima kwa nguvu bila majadiliano wala kushirikisha jamii kwa mazungumzo leo hii wananchi ni matajiri kwa kutegemea mazao hayo waliyolazimishwa kulima kwa nguvu.

    Ukilazimisha watu wapande miti kwenye eneo kama hilo sidhani kama ni ukoloni! Kama ni ukoloni basi ukoloni huo ni mzuri na unahitaji kupigiwa makofi!

    Society mara ingine zinahitaji kusukumwa ili ziendelee na zifanye mambo ya maendeleo.

    Kwa kumalizia nakumbuka nilisoma mahali kuwa mchaga akifia mbali na uchagani mtu hutakiwi kutoa mchango wa mawazo kwenye huo msiba kwani hakuna atakayekusikiliza bali watakuzomea tu sababu wanaamini mchaga akifia mbali na kwao kinachotakiwa ni mchango wa PESA za kusafirisha maiti siyo mchango wa mawazo sababu mawazo hayawezi kusafirisha maiti!

    Hapo Iringa milima hiyo inahitaji miti haihitaji mawazo yawe ya society au viongozi bali inahitaji miti.

    koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Wed Aug 29, 01:20:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Analyist, nadhani Tanzania ya uchiriku haina nafasi kabisa.

    Nakubaliana na Koloboi kwa mtundiko wake.

    Binadamu alizaliwa kwa starehe/kupumzika, na anapenda starehe na kupumzika. baadhi usipowalazimisha kufanya yale yenye faida kwao, nadhani hata wengine nguo zao hawatazifua.

    Hivyo Analyst, anapaswa kuachana na zile fikra za maongezi (Siasa)

    Mabadiliko ya maendeleo yataletwa nasi watanzania, Wasomi wachukue nafasi zao.

    Tatizo.

    Nadhani kuna wasomi wavivu na magoigoi. Hawa huangalia VYETI, badala ya ufanisi.

    Wapo wasomi, wanaoumwa na roho wanapoona hali kama hizi za uharibifu wa mazingira nk. Na wanatoa muongozo ili kwa wasimamizi (wahusika kwani ni wajibu wao.

    Mfano ulioutoa nadhani ni mzuri kwa kizazi hiki. Tunahitaji shughuli ifanyike sio blabla.

    Vitalu vya miche vipo vingikaribu kila mkoa.

     
  • Date: Wed Aug 29, 01:29:00 PM EAT, Anonymous Perez

    Naungana na Anony mmoja hapo juu kwamba kuna watu wengine humu wanafikiri kila vile vi theoriz theoriz na vi prinsipoz prinsipoz walivyofundishwa madarasani basi vyote ni PRAKTIKO kwenye ril laif.
    Vingine ni for academic purposes tu kwa ajili ya kufundishia. Eee!
    Shauri zenu!

     
  • Date: Wed Aug 29, 02:21:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Wanakijiji, kama nilivyosema hili niko tayari kuliandikia kurasa nyingi tu, mpaka kieleweke!! Siyo mambo ya theory wala nini. It is a practical matter whose fulfilment I have had the pleasure to witness!!!

    Sasa anon na Perez mkifuatilia historia mtaona kuwa kadiri siku zinavyokwenda ndivyo matumizi ya nguvu yanakosa "efficiency" na "effectivenness" dhidi ya mwanadamu yeyote awe Mmarekani, Mmongolia au Mzimbabwe.

    Jaribu katika familia yako. Kuna mambo wazazi wako walikuwa wakikulazimisha unafanya, sasa hivi mlazimishe mtoto wako uone kama atatii. No way!!

    It is a social transformation all over the world. Hata wazazi wanajua, mbinu za kuwalea vijana wao kwa sasa ni tofauti na walivyolelewa wao. Involvement in decision making! Pia viongozi wanaolijua hili wamaejikita kusoma zaidi kuhusu jamii laa sivyo hakuna kinachoweza kuwa achieved. The best CEO is not one who knows what to do but how to do what he does not know in order to know it.

    After all mazingira ni kwa faida ya nani? Si ya mwananchi? Kwanini um "by-pass" au kumlazimisha mambo yake mwenyewe? Tuache element za uongozi wa kikoloni. Africa is for Africans! Our own will and know how prevails, mambo ya nje ni kujazia nyama tu.

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Wed Aug 29, 04:17:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    KOLOBOI HONGERA KWA USHAURI MZURI,PEREZ NA WEWE NAONA SASA AKILI IMEANZA KUCHEMKA VIZURI NA WEWE HONGERA.

    ANALYST SIJAKUELEWA VIZURI UMEONGELEA NINI HASA.NAJITAHIDI KURUDIA RUDIA KUSOMA ULICHOANDIKA NAONA BADO SIKUELEWI VIZURI UNACHOSEMA.

     
  • Date: Wed Aug 29, 04:25:00 PM EAT, Anonymous Mliakuvana

    Katika somasoma yangu kwenye topic hii nimeona kuna mambo kadha ya kadhaa ambayo nadhani yamesahaulika.

    Jambo la kwanza naona watu wengi tumekimbilia kutoa solution without toaring causes (although we do know that kukata kuni kwa kupikia, kuota etc ndio iliyouweka milima hii katika hali yake ya sasa kama hiyo picha hapo juu)

    Jambo la pili, je hatuwezi kulishambulia tatizo (cause) ya hili swala kwanza kabla ya kukimbilia solution halafu ndio tukae na kuelimishana? Nilipita maeneo ya Ilula mwaka jana hali haikua nzuri sana manake mvua iligoma kuendelea kunyesha - mahindi yalikuwa ndio yawe yamebeba lakini yalikuwa yamesinyaa ile mbaya.

    Katika kuelimishana wananchi wa Ilula waulizwe wana matatizo gani kwanza. Nasema hivi kwa sababu sisi tulio nje tunaweza kuona mlima hauna miti kama zamani basi lazima kuna tatizo, kumbe wao wenyewe wasione tatizo lolote lile! Kama tatizo ni uhaba wa mvua, uhaba wa energy ya kustahimili maisha, uwingi wa mifugo, uharibifu mwingine wa mazingira etc etc basi waulizwe kwa nini ni hivyo.

    Tuelimishane kuwa mwanakijiji unataka kuni za kupikia na kujiweka warm during the cold months kwa hiyo unakwenda kata mti (na isitoshe hupandi mwingine!) In the long run mliokuwa mnauona msitu mkubwa ghafula hauna miti. Milima na miti husaidia katika "kupumua" kwa mazingira (si tunakumbuka zile diagram za mpaka mvua kunyesha? Sijui osmosis, precipitation, warm air rising, trees emitting Co2 etc etc)kazi sisi tulioenda shule kupeleka wanakijiji shule na sio kuwatapeli na kuwadanganya. Kwamba kutokuwepo kwa misitu kunaathiri kubadilika kwa hali ya hewa, sasa nyie wanakijiji mmekwenda kata kuni bila kupanda miti mingine, na kwa sababu hizo hapo juu mvua zimekataa, mifugo inakufa, mahindi hamvuni vizuri tena, umasikini unaenea, maisha bora kwa watu wote inaonekana ni ndoto!

    Tatu, what alternatives are we offering? Are there any? Are they feasible? Affordable? This is where the debate for alternative energy should come in, pronto! Just down the road in the little big town of Mafinga there is a Lutheran vocational college that specializes in making majiko that uses sawdust, and sawdust is abundant in Iringa region, and/or even mabaki ya mpunga can work. For light, the same college makes affordable solar light units.

    And, yes, another solution is campaign za kupanda miti vigorously lazima zirudishwe especially in those areas hard hit.

    Sio mbaya kuangalia wenzetu wa sehemu zingine duniani wanafanya nini. Bofya hapa na angalia kama kwetu itafaa au la. http://www.unl.edu/nac/brochures/wtc/wtc.pdf

    Apologies for the long post........

     
  • Date: Wed Aug 29, 05:32:00 PM EAT, Anonymous Makafoo

    Analyst,
    Hapa unatwanga maji kwenye kinu. WTZ ndivyo walivyo zimamoto kila kitu. Huwezi kukurupuka na kwenda kupanda mti kwenye mawe yale ukitegemea mvua za miezi mitatu halafu mti huo utegemee utasitawi wenyewe.
    Kampeni hizi za ajabu ajabu tumeziona miaka nenda rudi wakubwa wamefanya, mara mwaka huu kwenye mbio za mwenge imepandwa miti millioni ishirini. Rudi baada ya mwaka mmoja utakuta miti elfu moja ndio imebaki nayo baada ya mwaka mmoja huioni tena. Mara sijui wakati wa matembezi ya mshikamano tutaadhimisha kwa kupanda miti, hakuna kinachoendelea.
    Kama tunataka maeneo hayo yarudie hali ya asili ni kumilikisha watu. Hata kama wewe Koloboi unataka nenda pewa eneo hilo otesha miti. Tena kwa sasa utalipata kirahisi mno kwani watu wanaona halina faida.
    Bila kumilikisha watu tutaona uharibifu unaongezeka tu. Sasa hivi kila anayetaka kujenga kibanda chake anakimbilia Ipogolo. Matokeo yake hiyo milima itajaa makazi duni kama ilivyo milima ya Mwanza na hapo ndipo utakuwa mwisho wa ndoto za kukijanisha milima hiyo.

     
  • Date: Wed Aug 29, 06:18:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    ..........sasa inabidi shule zetu tuwe tunsfundis lughs ya KICHINA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

     
  • Date: Wed Aug 29, 06:42:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Makafoo nakushukuru sana. Nimefarijika kuona kwamba umeweza ku analyse jambo muhimu kati ya yote yaani milki ya ardhi!!

    Hizi siyo enzi za kufanya vitu visivyo na faida hata kidogo. This is an incentive-driven world. Yaani kiujumla ujumla tu wanachi wajitolee kulea miti milioni kadhaa iliyopandwa bila mpango kwa kampeni? No way my friend! Mtu hajala, watoto wake wanahitaji kutibiwa kwa gharama, hajui kama mvua itanyesha kukuza mahindi yake au laa umlazimishe atunze miti mlimani, ya kazi gani??


    Put yourselves in the shoes of these local peasants. Hii ndiyo assignment ngumu kuliko zote kwa viongozi na wasomi. Simshangai anon aliyesema analyst sikuelewi, its true, huu ni wimbo mpya. Tumezoea serikali ikitaifisha, ikimiliki kila kitu, na ikitoa amri fanya hili fanya lile. Gone are those old good days my friend.


    Swala la milki ya ardhi ni muhimu sana, iwe kwa mtu binafsi, kikundi cha watu au kijiji.



    Nitoe mfano, akitokea "venture capitalist" tuseme labda ni Mtanzania mwenzetu huku ughaibuni kapata pesa zake, akija Iringa mpeni mlima mmoja wapo. Aanzishe camp site wanafunzi wa vyuo vikuu wawe wanakuja huko mlimani wanajisomea na kupata burudani. Pole pole watalii nao waanze kupanda hata mmoja kwa mwaka. Atafanya kila awezalo kuukijanisha huwo mlima hata ikiwezekana wote!!



    Mifano mingi iko kaskazini mwa Kenya, mpakani na Somalia kwenye Jangwa. Lakini tusiende kote huko. Wanaoujua mkoa wa Arusha waniambie kama kuna "jangwa" linaloshinda eneo la duka bovu njia ya kwenda Minjingu. Maeneo jirani na snake park watu wamemilikishwa ardhi na kubadilisha kabisa jiografia ya hilo eneo. Ni kijani tupu!


    Kasi inaendelea maana kuna watu wa kuwaiga. Njia ya kwenda Namanga utakuta vijisehemu watu wameanzisha mashamba ya mbuni sijui nini na nini its all green. Ni maeneo ambayo hapo awali watu waliyakimbia kwa kuwa mifugo iliharibu kabisa hamna hata nyasi.



    Anon uliyezungumzia alternative energy hongera sana. That is the kind of thinking we want reinforced maana wanachi hawajaelimishwa. Sikuwa na information kuhusu chuo hicho cha Mafinga.

    Sasa wanachi hawawezi kuhama tu ghafla kutoka kupuliza moto wa mafiga hadi kutumia jiko la pumba. Again this is a cultural aspect. Kama ulivyosema wanachi waulizwe jamani eeeh, nyie mnatakaje??


    Nitaendelea kutafuta link za makala na kuzitundika hapa kwa wanaotaka kusoma zaidi.

     
  • Date: Wed Aug 29, 09:20:00 PM EAT, Blogger mwalyoyo

    UTANGULIZI

    Nawapa hongera wanakijiji kwa kuamsha mijadala mizito namna hii, lakini naona bado hatujafikia mwafaka wa namna gani tutekeleze suala hili, ili mawe hayo yatokomee kwa kumezwa na mimea. Najua mwafaka utapatikana tu hapa hapa kijijini, kwani sisi wanakijiji tunatofautiana mitazamo na tuna ujuzi wa namna anuwai, haya yote ni katika kufanikisha malengo haya.


    HOJA
    1. UMILIKI BINAFSI
    Kimsingi naunga mkono wachangiaji wanaosema kuwa hakuna mtu anayeyajua vyema, nje ndani mazingira ya hapo Ilula kwenye mawe kama wenyeji wenyewe wa mahali hapo. Hii iwe ndio hoja ya msingi kabisa katika kutafuta utatuzi wa janga hili la uharibifu wa mazingira, na iwe ndio chanzo cha kutafuta ufumbuzi, sio wa eneo hilo la Ilula tu, lakini hata kwa maeneo mengine ambayo yameathiriwa kama hilo. Naamini ufumbuzi utapatikana kwa kuwashirikisha hao hao wenyeji wa mahali hapo, kama wachangiaji walivyofafanua hapo juu. Kwamba, waliokata miti kwa ajili ya kuni, mbao, ujenzi, uchomaji wa mkaa na kadhalika huenda hawakutoka mbali na hapo, kwa hiyo ni hao hao. Kwa hiyo basi, naunga mkono hoja ya wao kushirikishwa katika kuhuisha mimea ya eneo husika. Hali kadhalika naunga mkono hoja za wachangiaji wenzangu, kuwa eneo husika liwe chini ya umiliki binafsi, tuache habari ya mali ya umma (Tragedy of the Commons), kwani haina uchungu. Watu wakimilikishwa maeneo haya watayaheshimu na watachukua hatua kwa wale wanaoyaharibu. Mfano mwingine wa mbinu shirikishi, kwa kujazia kwa Analyst ni mradi wa CAMPFIRE, ulio nchini Zimbabwe. Unaweza kusoma zaidi habari zake kwa kufuata kiungo hiki "http://www.resourceafrica.org/documents/1993/1993_campfire_bg.pdf".

    2. TUSICHANGANYE SIASA NA UTAALAMU
    Nimuunge mkono mwanakijiji anayeponda suala la kampeni za zimamoto za kupanda miti (potiticizing technical problems). Nami nashindilia misumari katika jeneza la kuzikia kampeni hizi za zimamoto. Kwa uzoefu wa nchini mwetu,mahali pengi katika nchi yetu kampeni hizi za zimamoto zimefeli, kwani watu wengi hujiandaa kwa siku hiyo tu, kampeni ikishapita na suala linasahaulika. Tusitarajie mbio za mwenge ama siku ya mazingira duaniani kutatua tatizo hili, hizi ni siasa, kamwe hazitengamani na hali halisi ya tatizo. Analyst na Makafoo nadhani wamefafanua vya kutosha tatizo hili. Kwamba tupande miti kwa sababu mwenge unapita ama ni siku maalumu hata kama hali hairuhusu, ni uendawazimu. Suala hili linahitaji utatuzi wa kitaalamu na sio siasa, na kama nilivyosema, wataalamu wa mwanzo kabisa ni hao wenyeji wa maeneo hayo yaliyoathiriwa. Baadaye sasa, mbinu za utaalamu za kisasa zichanganywe na uzoefu wa wenyeji hawa ili kuleta matokeo bora. Pia nichukue nafasi hii kupinga suala la kuanza kukurupushana na serikali kuu ama za mitaa wakati huu, kwani tutarudi kule kule, kama mwenzangu mmoja alivyochangia, kuweka vikao ili katika vikao hivi tujadili mahali kwa kwenda kufanyia vikao vya kutatua tatizo hili bila kuwashirikisha wakaazi wa eneo husika.

    3. MLISHONYUMA
    Kwa sababu wataalamu wa kwanza na wa kuaminika kwa mtazamo wangu ni wanakijiji wa eneo husika, naamini wao ndio wanaojua ni miti ama mimea ya namna gani ilikuwa inastawi katika eneo husika. Kwa hiyo basi, iwapo wazo ni kurejesha mimea katika eneo husika, sio vibaya kama ile mimea ya mwanzo (original indigeneous species)ikapewa kipaumbele,ndipo mimea mingine (exotic species)ipewe nafasi. Inawezekana mimea ya mwanzo isikubali katika eneo husika kulingana na ukubwa wa athari, lakini pia mimea vamizi ina athari zake, na huenda isistawi vyema. Inabidi tuwe makini na hili, kwani tusije kurudi kule kule, leo tunapanda mikaratusi, kesho tunaambiwa tukate kwa kuwa inaharibu vyanzo vya maji. Aibu!


    4. MCHANGANYIKO WA MBINU
    Kwamba tunapanda miti ili kutokomeza mawe ya pale Ilula isiwe ndio hitimisho la janga hili. Inabidi tuwasaidie wanakijiji wa eneo husika kuwa na majiko sanifu yanayotumia kuni kidogo sana, ili hata kama watakata miti hapo baadaye kwa ajili ya kuni basi kasi ya ukataji iwe ndogo kuliko urejeshaji. Suala la kukata miti kwa ajili ya kuni halikwepeki kwa mazingira kama ya Ilula, na kwa Tanzania inayofanana na Ilula, najua kuna baadhi watapinga, lakini kabla ya kupinga tujiulize, ni wangapi tunatumia majiko ya umeme majumbani kwetu? Ni wangapi tuna uhakika kuwa umeme leo hautakatika kabisa? Je bei ya mafuta ya taa ikoje? Je huyu mwanakiji anatumia jiko la mchina kama wewe wa mjini? Je anaweza kununua mkaa kama wewe?

    5. MCHANGO WA HALI NA MALI

    Ilula ni eneo moja tu kati ya maeneo anuwai ya nchi yetu yaliyokumbana na athari za uharibifu wa mazingira. Sema bahati nzuri kwamba lipo njiani na hivyo limepigwa picha kiasi kwamba tumeliona. Na kama ilivyo ada, Mtanzania anaruhusiwa kuishi popote pale ndani ya Jamhuri yetu, kwa hiyo basi huwezi kujua lini na wewe siku moja utajikuta upo Ilula, ama lini hapo kwako pakawa dampo lenye athari mbaya zaidi ya hizi tunazojadili. Kwa maana hii suala la kusaidia eneo husika ni la sisi wanakijiji hiki pamoja na wengine wote, kwa kishirikiana na wanakijiji wa Ilula. Wamiliki wa Ilula ni sisi sote! Tujitoe kwa kila hali na mali kufanikisha suala hili. Niko tayari kutoa mchango wa hali na mali tukimaliza mjadala huu. Bw Mjengwa kaweka mawasiliano hapa kijijini, nitawasiliana nae!

    HITIMISHO
    Ndugu wanakijiji wenzangu, kama kamera iliyotumika kupiga picha hii ya mawe ya Ilula ilinunuliwa kwa michango ya wanakijiji, kwa nini isiwezekane kubadili eneo hilo pichani na mengine yaliyoathirika kama hilo kwa jina la kijiji hiki? Jamani, hii ndio kazi ya kijiji hiki, kuikomboa Tanzania kwa namna yoyote ile. Kwamba, mwisho wa mjadala huu iwe ni mwanzo wa utekelezaji wa mawazo haya ya wanakijiji.

    Wananakiji wenzangu naomba kuwasilisha!
    http://jadili.blogspot.com

     
  • Date: Wed Aug 29, 09:55:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Mwalyoyo, now you are talking! Nitakutembelea pia kijini kwako sikuwa najua njia!
    Naunga mkono hoja "to walk the talk" vinginevyo nasisi tutageuka wanasiasa pori!

     
  • Date: Thu Aug 30, 12:21:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Mimi naona wanaongelea ubinafsihaji hiyo milima na kung`ang`ania kuwashirikisha wananchi naona kama watu wanaoimba classroom songs au wanaotoa classroom textbook solutions.

    Ubinafsishaji wa hiyo milima hauhitaji kuiomba serikali iruhusu.Serikali ilisharuhusu. Wewe kama ni mwekezaji wa kilimo kiwe cha misitu au miti milimani nenda hata leo Kituo cha uwekezaji ukalipe mamilioni ya kulipia hiyo ardhi ya milima Iringa watakupa hiyo milima uweke hivyo vitu unavyotaka kuweka wakiridhika na hiyo miradi yako na uwezo wa fedha na mtaji ulionao.La muhimu ujue hutapewa bure kama mwekezaji hiyo milima.

    Kama Analyist na wengineo mnachoongelea kuhusu hiyo milima kupewa watu binafsi au makampuni mnamaanisha kuwa serikali iwape wawekezaji binafsi nawahakikishia hilo halihitaji Mjengwa aende akazungumze na mkuu wa mkoa wala mbunge. Ni suala tu la mtu anayedhani aweza pata faida kwa kuwekeza kwenye hiyo milima afanye kwenda serikalini aombe hiyo ardhi akipewa ailipie hiyo ardhi haraka na atuambie wanablogu atakamilisha lini huo mradi wake tuache kuisumbua serikali na hiyo milima.

    Uwekezaji kwenye ardhi Tanzania unaruhusiwa uwe wa mabondeni au milimani mradi tu kama una pesa za kulipia hiyo ardhi na mtaji na investment proposal inayokubalika.

    Kama wewe Analyist na wenzio mnataka milima hiyo imilikiwe kibinafsi au na kampuni au jamii fulani kama wawekezaji mtupe muda lini mtaenda kulipa mamilioni ya pesa kwa serikali mpande hiyo miti au muweke hivyo vitega uchumi vyenu kwenye hiyo milima yenye mawe matupu Iringa.Hiyo mifano ya nchi mnakosema watu binafsi wanamiliki hayo mashamba ya miti na milima kama hiyo ya Iringa kwa taarifa zenu hawakupewa bure ardhi hiyo waliuziwa na serikali baada ya kulipa mamilioni ya pesa. Pamoja na kuwa mlieleza juu kwenye hii blogu mkiwasifia sana watu binafsi hao utafikiri hizo ardhi walipata bure!

    Mheshimiwa Analyst, Tanzania kama unataka hiyo ardhi ya milimani ili uwekeze mamilioni ya pesa ya mtaji nenda serikalini na proposal yako uiambie kuwa wewe ni mwekezaji unataka kuwekeza kwenye hiyo milima wakiikubali proposal yako watakupa hiyo ardhi ya milima ya Iringa baada ya kulipia mamilioni unayotakiwa kulipa kupata hiyo ardhi ili uweke hivyo vitega uchumi hewa na vitega uchumi blabla unavyoongelea wewe Analyist na wenzio kwenye hii blog ya mjengwa.

    Mjengwa tusaidie kuwaomba akina Analyist watupe time frame ni lini hiyo miradi blabla yao ya uendeshaji kibinafsi itakuwa tayari kukamilika maana hatuwezi kuongea na kuongea na kuongea kama tuko kwenye simu za mkononi za TIGO,CELTEL au VODACOM lazima tufikie mahali miti ipandwe kwenye hiyo milima.

    Kuhusu kusema kuwa lazima jamii ishirikishwe sababu jamii yenyewe ndio wafalme ! Nadhani Somo la Social Markerting limewapita pembeni baadhi ya waheshimiwa kwenye hii blog

    Labda nifafanue kidogo Ni lini jamii ni wafalme na lini jamii si wafalme katika mradi wa kijamii? Ni somo refu ila nitaongelea pande mbili tu kwa kuokoa urefu wa hoja:

    Kwa kawaida huwa kuna mashirika yenye kutoa mapesa ya bure kwa ajili ya miradi ya kijamii kama huo wa kupanda miti mfano.Sasa ili kupata hizo pesa za mradi kutoka kwa wafadhili sharti moja la kupata pesa kama hizo huwa ni kuwa lazima mradi huo ubuniwe na uhitajiwe na wananchi wenyewe kwenye lile eneo ili pesa zitolewe na wafadhili.Hapo ndipo jamii ya mahali huwa wafalme sababu bila wao kusema ndiyo pesa kwa mfadhili hupati.Walimu wa theory ya pesa za ufadhili na miradi ya kijamii ndio hukazia sana suala la jamii kuukubali mradi kabla ya kuutekeleza.

    Lakini kuna Upande mwingine mfano jamii hiyo ya Iringa mjini iliyo karibu na misitu ya milima wameleta athari kwa watu wengine kwa kusababisha wakose mvua kwa sababu ya kukata miti.Ina maana kutojali mazingira kwao kunaleta athari kwa watu wengine wakaao hata mbali sana na hapo mjini uharibifu wa mazingira unapofanyika.Watu wanakosa hewa nzuri na mvua sababu ya wakazi wa Iringa mjini.Hapo huhitaji kujikomba kwa watu wa Iringa Mjini kama wanataka au hawataaki kupanda miti.Hapo ndipo kazi ya serikali huingia kushinikiza mradi na kuangusha utawala wa kifalme wa jamii.

    Yawezekana kabisa mfano ukienda Iringa Mjini waweza ukuwauliza kama wanataka huu mradi wa kupanda miti mlimani wote kwa kauli moja waweza kusema hatuutaki lakini pamoja na kukataa kwao lazima miti ipandwe ili kunusuru jamii zingine nyingi zinazoathirika na vitendo vya uharibifu wa mazingira wa watu wa Iringa mjini.

    Kwa kumalizia Analyst na wenzio mjue kuwa kwenye suala la mazingira society ya mahali siyo pekee yenye sauti ni lazima maslahi ya societies zingine yazingatiwe pia.Kwani uharibifu wa mazingira wa society moja huathiri society zingine dunia nzima ikiwemo kuongezeka joto duniani.Kudhani society ya Iringa mjini tu ndiyo yenye uamuzi wa mwisho wa mradi wa mazingira wa kupanda miti si kweli.

    Na kwa hali ya mazingira ninayoiona kwenye hiyo milima hakuna haja ya kuwabembeleza hao wakazi bali ni kulazimisha miti ipandwe sababu uharibifu huo unaathiri wengine ndani na nje ya Tanzania kwa kuchangia ukosefu wa hewa safi, mvua,na kuongezeka joto na jangwa duniani.

    koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Thu Aug 30, 09:01:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Akina Analyst,Mwalyolo,na Makafoo kwangu mimi nadhani ni walimu wa Miradi ya Kufikirika (Imaginary Projects) ambayo haipo na haitekelezeki ila inazunguka mawazoni kichwani kwa mtu aliyeko darasani.Miradi kama hiyo Iringa hatuihitaji.

    Kama wana pesa wawekeze basi! sioyo ooh! Wapewe watu binafsi. Ni akina nani hao watu binafsi! Wako wapi miaka yote hiyo? Je Wana uwezo wa kununua hiyo ardhi na kuilipia kila mwaka serikalini kodi ya ardhi wakipewa hiyo milima? Au wanaongea tu kufurahisha baraza na kupoteza muda wa wana blogu.Kama wanawajua watu hao binafsi wenye uwezo wawalete Iringa na watupe ripoti kwenye hii blogu ya uwekezaji si wa kwenye milima bali hata wa kichuguu walioufanya.

    Naungana na Koloboi kuomba tupande miti tuache blabla.

    Kama hawajajitokeza hao wawekezaji binafsi hadi leo tuanzishe kampeni haraka masika ya mwaka huu tupande hiyo miti wananchi wa Iringa tusisubiri wawekezaji binafsi wa milimani wasiokuwepo.

    Mimi naona mawazo ya Koloboi yaweza wezesha miti kupandwa mwaka huu kama dhamira ya viongozi wa mkoa huu ipo.

    Kuhusu utunzaji wa hiyo miti napendekeza kila chama cha siasa kipewe mlima mmoja kitunze hiyo miti.Sababu kama chama kinaweza kutunza miti naamini kinaweza tunza watanzania.Ikishaoteshwa miti CCM,CUF,CHADEMA,TLP,DP,NCCR ,DEMoKRASIA MAKINI n.k kila kiongozi wa Chama mkoani petu hapa apewe eneo na wanachama wake watunze miti.Wengi hatujui kazi za vyama nini nadhani wakitunza miti tutajua kazi zao ni pamoja na kutunza miti.

     
  • Date: Thu Aug 30, 01:04:00 PM EAT, Anonymous Mliakuvana

    Maggid, naomba hii picha, na zile picha tatu za Ipogolo, Ndiuka na chuo cha maendeleo Ruaha, na zile za Iringa mjini uzipige tena mwezi January 2008 ili tuweze kucompare.

    Naelewa zimepigwa wakati huu wa kiangazi hence the golden hue. I am kinda curious to see the contrast in vegetation and color if the rains come. Inawezekana nitaona mwenyewe nikienda "kuhiji" December!

     
  • Date: Thu Aug 30, 02:27:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Suala la kupanda miti na kutunza mazingira kwa ujumla wake, ni maelekezo tu, na kuhamasisha wanachi kufahamu maana na faida kuotesha miti.

    Mara nyingi, wananchi huweza kuwa na mawazo kuwa shughuli fulani ni ngumu na haina faida, lakini akielimishwa au akioneshwa mfano anaelimika na anaweza kufanya maajabu.

    naongana na Koloboi, NGONJERA sasa basi, TUFANYENI KAZI, wasomi, wataalamu chukueni nafasi zenu. Ancheni KUTISHWA hawa wana POROJO, ambao wanashindwa hata kufahamu ni nini hasa maana ya UONGOZI.

    Nilimuuliza mmoja aliyejiita kada wa Chukua C. badala ya kujibu AKANG'AKA, ukali wa nini unaulizwa swali jibu swali.

    WANAKIJIJI WENZANGU hii mada nzuri sana na inawachangiaji wenye mawazo yanayoshawishi. Nikiwa na maana hata yale yasiyotekelezeka, yanakuwa na mvuto kuyasikiliza.

    TUKIMALIZA HILI NAWAOMBA TURUDI KATIKA HILI LA MIFUKO LAINI YA PLASTIKI.

    NAKUMBUKA AWAMU HII YA NNE, ILIINGIA NA MIKAKATI YA KUITOKOMEZA

    Mshangao, MIFUKO HII INAZALISHWA NA INAHARIBU MAZINGIRA VIBAYA SANA.
    Hili ni dhaifu jingine la uongozi wa MATAMKO.

    Tutekeleze mikakati tuliyojiwekea kwa VITENDO.

    Tuseme blabla SASA BASI

     
  • Date: Thu Aug 30, 02:31:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Mliakuvana,

    nadhani lengo hasa la siyo kijani cha nyasi, TUNATAKA KIJANNI CHA MITI (MSITU)

     
  • Date: Thu Aug 30, 10:20:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Kabla sijaendelea naomba kupongeza sehemu ya maoni ya Koloboi, nitanukuu "...uharibifu wa mazingira wa society moja huathiri society zingine dunia nzima ikiwemo kuongezeka joto duniani"

    Hapa hata dhamira itanisuta nisipo comment kwamba umeonyesha uelewa wa principle muhimu sana ya kimazingira. Chini ya hii kuna principle nyingine "state sovereignty" na chini yake tena "community involvement"

    Mazingira ni ya dunia nzima lakini kila nchi inajiamulia ifanyaje, kila nchi pia inatakiwa iwa involve local communities. Mikataba yote ya KISASA ya mazingira duniani imeundwa kwa kufuata mfumo huu.

    Jambo tusiloelewana humu kijijini na sishangai ni kuhusu "property rights" ni mfumo mpya kiasi!! Kama kuna tawi lolote la AWF ama WWF hapo Iringa waulizeni watawaambia zaidi.

    Kutaja "venture capitalist" ni mfano tu kuonyesha jinsi "tragedy of the commons" inavyoweza kurekebishwa kwa "ubinafsishaji". Otherwise kila tukisema miliki ya ardhi na mali asili hatuna maana ya kutafuta muwekezaji. Nani hajui kuwa hawapo??? Kila kukicha tunatafuta wawekezaji kwenye sekta za kilimo hawapo!! Wapo kwenye madini, misitu, utalii na kadhalika.

    Ninasisisitiza kuwa wanakijiji wamilikishwe hayo maeneo. Make them feel like it is their own property. Create a sense of belongingness. Anon aliyesema wapewe vyama vya siasa, it is EXACTLY what we are saying here. Mimi nilipendekeza watu wa vyuo vikuu ndiyo wapewe. Kama na vyama vinaweza kujumuishwa it is well and good!!

    At least someone must be identifiable na siyo ujumla jumla na ukampeni kampeni ama uzima moto zima moto. Hatuendi hivyo siku hizi my friend.

    Hata hivyo niko tayari pia kushirikiana na upande mwingine wa hoja kama ndiyo utashinda. Tutashirikiana na kupitia kijiji chetu tutajifunza hata baada ya miaka kadhaa kama tumefanikiwa au laa. Time will tell.

    Binafsi ninajua watu ndiyo wanabadilisha mazingira na siyo mazingira kubadilisha watu. If we are successfull in bringing back this lost link hata kama ni eneo dogo vipi, ni mafanikio ambayo ni endelevu yaani sustainable.

    Siyo ya miti kupandwa tu kwa vile tuko excited baada ya kuona picha zimetushtua. Hiýo milima iko hivyo kwa muda mrefu, panic will not help. Sisi tulioko nje tunaona kama ni ajabu vile so our pace may not necessarily be that of the concerned.

    Wewe ukionyesha kwamba umepanic unataka kuwahi mvua za mwaka huu ndiyo kwaaaaanza utakosa support ya wananchi ambao hawapendi zima moto. Think of sustainability!!!! Strategise!!!! Not how quick you do it but how long the impact will last. Kaaaaazi kweli kweli!

    Nawashukuru

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Fri Aug 31, 10:41:00 AM EAT, Anonymous Mliakuvana

    Anony wa Tarehe: 30/8/07 2:31 PM, ndio maana nimesema "vegetation" na hakuna anywhere nilipoema "nyasi"

    Vegetation: all the plants or plant life of a place, taken as a whole e.g. the vegetation of the Ruaha valley. (Dictionary.com)

     
  • Date: Fri Aug 31, 12:17:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Sasa nadhani twaweza sogea hatua moja mbele tuingie hatua ya pili baada ya kuongea na kuongea na kuongea ili tusiliache suala la hiyo milima hewani.

    Tunakuomba Mjengwa na wandishi wa Wahabari sasa mwende kwa uongozi wa mkoa wa Iringa, na Manispaa ya Iringa,Na Idara ya misitu hapo Iringa waulizeni watapanda lini miti kwenye hiyo milima na wana mkakati gani gani ya muda mfupi na mrefu ya kuhakikisha miti inapandwa kwenye hiyo milima na inastawi.Na wataanza kuitekeleza lini hiyo mikakati yao.Wakupeni time frame kabisa msikubali majibu ya jumla jumla yasiyokuwa detailed na action oriented.Wawape ratiba kabisa ya utekelezaji.Kama hawana tuleteeni taarifa tujue Kuwa mwaka huu hawana mpango wowote na hiyo milima tujue kimbembe gani kifuate.

    Majibu ya viongozi hao wa mkoa, manispaa na idara ya misitu yaje haraka kwenye Blogu hii watu tuyafanyie kazi upesi tuhakikishe milima hiyo inabadilika upesi hali yake.

    Koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Fri Aug 31, 08:34:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Kwa Koloboi...

    Nakupongeza kwa maoni yako hapo juu, lakini unajibu kwa jazba mno, kiasi kwamba unakuwa unarudia baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wachangiaji wa mwanzo. Suala la kukurupuka na na kuwahi mvua za masika litaturudisha kule kule tulikotoka. Lazima tufanye mipango madhubuti ya kuhakikisha miti hiyo inakuwa na inapata ulinzi wa kutosha.
    'Siungi Mkono' suala la kuanza kukurupushana na serikali kwamba ni lini watapanda miti eneo husika. Hawatatupatia majibu ya kujenga. Majibu utakayopatiwa ni kama haya:-
    a. Serikali inatambua na inakerwa sana na tatizo hilo na ipo mbioni kulitafutia ufumbuzi. Kwamba ufumbuzi utakuwa lini hawasemi!
    b. Serikali haina pesa kwa sasa, ila itaangalia uwezekano wa kutenga pesa katika bajeti ijayo ili kukabili tatizo hili.
    c. Serikali iko katika majadiliano na wafadhili kuangalia namna ya kupata pesa za kuoteshea mimea katika eneo hilo.
    Cha ajabu sasa, miti tulikata sisi, lakini kupanda tunataka ufadhili! Noma sana!
    Nakuunga mkono Koloboi kuhusu kwenda hatua ya pili, lakini hatua hii isiwe kwenda serikalini, iwe ni mpango kazi wa utekelezaji wa mradi huu wa kijiji.

     
  • Date: Fri Aug 31, 08:52:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Anon wa 31/8/07 10:41 AM nakuunga mkono. Twendeni hatua nyingine. Hakuna topic ambayo imenigusa binafsi kama hii tangu nianze kuja humu kijijini. Mazingira ni uhai.

    Usishangae kukawa na variation ya furaha ya ndani kati ya mtoto anayezaliwa kwenye mazingira yaliyo haribika na aliyezaliwa katika mazingira yanayotunzwa. Nisilete story (Ukimtembelea Freddy Macha utaona karibu agusie hili kuhusu nature).

    Tuonyeshe kukerwa kama wenye nchi na kama wazazi na wazazi watarajiwa. We can do something! Watoto wetu na wajukuu wetu waangalie rangi ya kijani, iwe translated katika mioyo yao kama hope!

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Fri Aug 31, 10:57:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Serikali msiigope kuiuliza wanablogu tunaiweka wenyewe kwa kura zetu na kuifanya iendelee kuwepo kwa kodi zetu.

    Wana haki kuulizwa na kutueleza wanablogu. Tujue wanaweza hilo swala au hawawezi.Kama limewashinda kuna haja gani wawepo kwenye hivyo vyeo vyao.

    Nchi zingine viongozi hutimuliwa uongozi na Raisi baada ya kupokea mapendekezo toka kwa wananchi yenye ushahidi wa wazi kuwa viongozi wameshindwa kazi ya kuwa wabunifu katika utekelezaji wa kazi za kila siku. Na sisi hatuwezi kuwachukulia hatua kama hatuna ushahidi wa wao kushindwa hiyo kazi.Ndio maana nikapendekeza wakaulizwe tuletewe majibu yao na majibu hayo tuyafanyie kazi.Wana uhuru wa kujibu chochote hata kusema hawana cha kujibu.Wajibu tu na tuletewe majibu.

    Anoy unayetaka kuwa msemaji wa serikali kwa kusema eti watasema hela hakuna ya bajeti mwaka huu! Huo ndio ujinga wa viongozi wengine wa Serikali .Unapopewa Cheo ni pamoja na kutatua matatizo ikiwemo kutafuta hela kama hazipo ili utekeleze miradi ya maendeleo.Kama umepewa bajeti ndogo au hukupewa inabidi uwe mbunifu wa kutafuta pesa pia utekeleze hiyo miradi.Sasa kama hujui kutafuta pesa unaongoza nini wakati unajua miradi inahitaji pesa? Ina maana kama miaka 20 hujapewa hela za bajeti ya maendeleo utakaa tu unatafuna pesa za walipa kodi kwa mishahara na posho tu.

    Watanzania tujue sasa kuwa wakati wa majibu rahisi ya kijinga umepitwa na wakati sasa watu wamesoma na wanaelewa waliyosoma tofauti na zamani ambapo watu walikuwa wanakariri masomo ili wapate vyeti.

    Nakuomba unayesema nina jazba Wacha watuletee majibu wenyewe usiwe msemaji wao.Hayo majibu tuyafanyie kazi.Usijali kama watatoa majibu ya kujenga,kubomoa,ya vitisho,ya kisiasa au ya kihuni,kiburi au ya vipi.Wacha tu wajibu wapendavyo halafu yaletwe hapa kijijini.Nakuhakikishia Kijiji kina watu wengi na penye wengi haliharibiki neno.

    koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Sat Sep 01, 12:05:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Mjengwa nataka nipande miti 100 wakati wa mvua za masika mwaka huu kwenye milima Iringa.

    Nimewasiliana na rafiki zangu huko Dar es salaam wamesema watanisaidia kuipanda kwa niaba yangu na watapiga picha eneo walilopanda na picha itawekwa kwenye hii blog muione hiyo miti.

    Mjengwa naomba ushauri ni miti gani inastawi huko,na miche yake inapatikana wapi na kwa gharama gani.

    Naomba uweke hili kwenye blog hii.

    Mimi mvua zangu za masika nina usongo nazo nataka kuzifanyia kazi lazima nipande miti 100 mwaka huu.

    koloboi@yahoo.com

     
  • Date: Sat Sep 01, 02:46:00 AM EAT, Anonymous ANALYST

    Koloboi katika kulijibu swali ulilomuuliza Mjengwa ndiyo tunaanza kufanya strategy ya kuwashirikisha wananchi na kuwasikiliza.

    Anon mmojawapo alilisemea vizuri kuhusu vegetation na kuwauliza vijana wa zamani ni miti gani ilifunika milima miaka hiyo.

    Mimi ningefurahi hao jamaa zako wakimsaidia Mjengwa kukutanisha ma babu, ma bibi, jamii nzima wazungumze halafu Mjengwa atuambie hapa jamii inafikiri nini. Ninasapoti sana kikao cha asili kuhusu kukijanisha mlima. Ikiwezekana watu wakae chini waki "sip" ulnzi wao, wazungumze kihehe, totally relaxed siyo mood ya zima moto wala kampeni. hakuna kupigiana makofi wala kuvaa tai. Ni kazi!

    Atafutwe facilitator anayejua huu wimbo. Hata mwaka huu tukiishia kuzungumza tu, haidhuru!!

    Tujenge urafiki na jamii pamoja na kufanya feasibility study, udongo au mawe ni kiasi gani, upepo unazoa "matter" kwa kasi gani na kadhalika. Pole pole ndiyo mwendo!

    Bila feasibility study ya kueleweka unaweza kwend na miti ukasahau kumbe ulitakiwa ubebe sururu badala ya jembe! Thigs are very different on the ground Mheshimiwa Koloboi.

    Nawakilisha wanakijiji.

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Sat Sep 01, 10:28:00 AM EAT, Anonymous Anonymous

    Taabu ya wasomi kama Analyst wanafanya kazi wakiwa wamekaa kwenye viti.Kwa hiyo kwa sababu ya kupenda kukaa kwenye viti wanapenda sana kukaa kwenye viti kwenye vikao visivyoisha vya ku-analysise.

    Koloboi kaomba apewe miti gani inastawi na inapatikana wapi mpeni data.

    Analyst anataka kikao na wazee wa zamani wa nini na vya nini hivyo vikao?

    Analyst unataka kutuambia data kama hiyo huwezi ipata idara ya misitu au kilimo hapo Iringa? hadi uanze kuitisha vikao tena kama ndiyo kwanza unaanza utafiti wa kujua miti ya hapo Iringa.

    Mpeni koloboi hizo data afanye kazi.

    Eti Analyst anasema atafutwe facilitator! wa nini? Au mna lengo la kumtengenezea kaulaji.Akipatikana apewe kanauli,Kaposho,Kausafiri,Kakomputa n.k hiyo miti itakuja pandwa kweli kwa staili hii ya Akina Analyst.

    Nyie wahehe wa Iringa mnataka mazungumzo au mnataka miti ipandwe?

    Mimi ni mkazi wa singida anayeishi Dar es salaam .Kwetu kuna tatizo kama hilo la Iringa.

    Nimewaambia nyumbani waangalie miti gani kule ya kupanda nitamwandikia Koloboi aje apande kwetu hata kama ni 20 tutamshukuru.
    Something is better than nothing.

    Mheshimiwa Koloboi nitakuandikia kwenye e-Mail yako.Tutafanyia kazi mawazo yako Singida.Usituchoke tukihitaji msaada wako.Karibu singida.Nitakutumia pia picha za hali zilivyo kule Singida.

     
  • Date: Sat Sep 01, 11:20:00 AM EAT, Anonymous ANALYST

    Anon wa 1/9/07 2:46 AM Nimekuelewa. Tatizo lako ambalo kwa kweli sikulaumu ni kwamba, kama walivyo watanzania wengine umechoshwa na mazungumzo yasiyo isha. Pili hupendi maneno kama "facilitator" Sikulaumu. Wenzetu wa mashirika yasiyo ya kiserikali wameharibu maana ya mísamiati hii ya kimaendeleo. Wanachi wamechoshwa na vikao na ulipanaji wa posho kwa mafacilitator. But wait a minute, there is still hope.

    Nikisema facilitator, ghfala mtu anapata picha ya mtaalamu kutoka Dar au Chuo fulani, mwenye compyuta anayelipwa nights na kadhalika. Siyo kweli. Facilitator anaweza kuwa balozi wa nyumba kumi wa hapo hapo Iringa. Afacilitate mazungumzo. Watu wawe huru kusema wanachofikiri. Siyo lazima alipwe. Anaweza asipewe hata shilingi kumi. You just acknowledge him or her.

    Tusikate Tamaa watanzania wenzangu. "Kuelewana ni kuzungumza". Jifunzeni kuzungumza na wanachi. Miti haijaanza kupandwa leo. Siyo Iringa, Singida wala Dodoma. Ila hali inazidi kuwa mbaya. Kwanini? Something must be wrong! Zima moto zima moto zimaoto plus compaign na kupigwa picha. Weka pembeni 'haraka haraka' and see the results.

    Kikao cha asili nitaendelea kukipigia debe hata wote mkinipinga. Lazima jamii ihusishwe katika kuleta mabadiliko endelevu. Naweza kuwa msomi ninayependa kukaa kwenye kiti but my heart moves to the community. It does not help how much you are "there" physically if mentaly and spiritually unawaona wananchi wamepitwa na wakati. Ni wavivu, wanahitaji kulazimishwa kufanya hili na lile. Ni ukoloni. Lets change some of these things my dear country men. I can say it is too little too late already but we must not lose hope. Lets do what is right.

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Sat Sep 01, 12:22:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Kama mnataka kujua watu wamechoka na uchiriku, someni mitundiko ya koloboi.

    Nakuapieni kwa jina la MUNGU ninayemfahamu na kumuamini, watu kama koloboi ni WAKOMBOZI. Hawa hawataki NGONJERA wanataka kazi. wanataka kuona jambo lililokusudiwa linatekelezwa.

    Analyist, hebu badilika kidogo, Tanzania ya leo hatutaki tena vikao, matako yanauma sasa kwa kukaa.

    Tumekuwa watu wa vikao na maneno kwa miaka mingi na ndiyo hali kama hii tunakuwa nayo sasa.

    Nilikwisha wahi kuuliza humu,
    Je! inawezekana kugeuza mbuga kuwa msitu/pori?

    SHUKRANI ZA PEKEE ZIMWENDEE Anony 1/9/07 10:28AM wa Singida kwani swali langu kwa asilimia 100% lilikuwa linalenga Singida.

    Analyst, TUTOKOMEZE ILE DHANA YA WATANZANIA MANENO MINGI.

     
  • Date: Sat Sep 01, 01:00:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Hivi AnalystMunge na Perez ni mapacha wa kuzaliwa pamoja?

    Naona kama hoja zao siku hizi kama zinafanana.Ukisoma za AnalystMunge utafikiri kaandika Perez na ukisoma za Perez utaziona kama za AnalystMunge.

     
  • Date: Sat Sep 01, 01:02:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Analyst,

    Sijui upo Tanzania au nje ya Tanzania.

    Popote pale ulipo, kama kunauwezekano wa kupata nakala ya gazeti la Rai la 23-29'2007, nitaomba usome ukurasa wa 19.

    Wadau wanasema limekwisha nunuliwa na RA sipingi, lakini huu ukurasa hauzungumzii si hasa.

    Unazungumzia ubunifu na Uthubutu.

     
  • Date: Sat Sep 01, 02:02:00 PM EAT, Anonymous Anonymous

    Ndugu Maggid Mjengwa,

    Naomba nitoe mapendekezo yangu humu kijijini.

    Iwapo uwezekano upo, hii picha (jinsi ilivyo) ya huu mlima uwe unaiweka kila mwezi. Nadhani itakuwa inawakumbusha wanakijiji kujadili na kuhimizana kutunza mazingira hasa yanayohusiana na upandaji wa miti.

    Halafu tutafute tena muda wa kutokomeza hii PLASTIC BAGS (Rambo) hasa hizi laini.

    Ningelikuwa na uwezo, ningetunga sheria ya atakayekutwa nayo adhabu yake iwe faini ya shs 15,000.00 au jela miezi miwili au zote kwa pamoja.

    Kabla ya adhabu hii kuanza, lipite tangazo kwa makazi yote Tanzania, kwa muda wa miezi miwili, Mabalozi/wajumbe na madiwani wote wahakikishe kuwa kila mkazi anaondoa masalia ya mifuko hii katika maeneo ya nyumba/kiwanja chake na kuichoma.

    Wazalishaji. Ni heri serikali iingie hasara ya kufidia viwanda vyote. vinavyozalisha, kuliko kuua ardhi yetu ambayo ndiyo chanzo kikuu cha kutupatia chakula.

    HII MIFUKO NI HATARI.

    MAKAMU WA RAIS, TUNAKUTEGEMEA KUMSAIDIA RAIS KUTOKOMEZA UCHAFU HUU MBAYA.

     
  • Date: Sun Sep 02, 01:16:00 AM EAT, Anonymous ANALYST

    Anon wa Hawa1/9/07 12:22 PM Ukielezea kuchoka uchiriku na kumsifu Koloboi umesema, nanukuu "hawataki NGONJERA wanataka kazi. wanataka kuona jambo lililokusudiwa linatekelezwa." Sikatai. Nani kasema mkiongoea mtagoma kufanya kazi? Jee huwo uchiriku unaozungumzia unahusiana na kazi? Sijawahi kuona kazi yeyote endelevu inayofanywa bila ku-strategise. Kuzungumza ni kuweka strategy. Kama previous experiences zimeonyesha kuzungumza hakuna faida siyo lazima ukomo wetu uishie hapo. Mabasi yanapata ajali kila kukicha, je watu wameacha kuyatumia kwa usafiri? Dont block the way due to previous failures, there is still hope!

    Anon wa 1/9/07 1:00 PM Nafikiri hakuna ubaya wowote kunifananisha na Perez. Anatoa mtizamo mbadala na huenda ni kivutio kikubwa humu kijijini. Tujifunze kuwa accomodate watu wa aina tofauti na sisi. Diversity is strength!


    Anon wa 1/9/07 1:02 PM Niko nje ya nchi. Naweza kusoma magazeti yaliyoko mtandaoni tu. Hayo mengine tunategemea wasamaria wema kama Magid kutuwekea japo kurasa moja moja humu.

    Tatizo lingekuwa kupanda miti wala watu wasingehangaika sana. Kwa mfano, ingekuwa tatizo ni hiyo miti ya 100 ya Koloboi kuingia ardhini mapema iwezekanavyo, sidhani kama inashindikana kutafuta vijana kama kumi hivi, wasio na ajira mjini ukawalipa elfu mbili mbili wakakimbia mlimani kuipachika hiyo miti.

    Wenzenu tunajaribu kufikiria mbali zaidi. Kazi ifanyike, Yes, lakini ionekane imefanyika na iendelee kufanyika. We are thinking in terms of perpertual growth and sustainability.

    Miti isipo ota tujue tunamuuliza nani. Miti isipo tunzwa tujue mwakani tutafanyaje ili kujirekebisha. Kwa sasa kuna gap kubwa sana kati ya wanaotoa amri na wanaopaswa kutekeleza hizo 'amri'. Anayetambua ukubwa wa tatizo hili hashindwi kuinvest zaidi katika kuwa karibu na wananchi.

    Hao wanasiasa na hata watu wa kawaida, wanaojipatia umaarufu kwa kuponda mazungumzo kuwa eti ni ngonjera, ni uchiriku, wataiharibu nchi kuliko walivyoikuta. Hakuna dereva anayeweza kujisifu kwa kukimbiza gari spidi huku amewaacha abiria nyuma. Ninarudia tena ile equation yangu. Change an individual then the society then the environment. Dont try to do the other way round, it wont work! Usipande miti milioni moja at ago kwa zima moto ukafikiri utakuwa umeibadili jamii, NO WAY!

    Tuonane tena jumatatu. Hoja zinazonihusu nitajaribu kuziaddress.

    Nawashukuru sana wanakijiji wenzangu. Kuna mwenzetu siku hizi anamalizia ENE WEI TUTAFIKA TU!! I like that!!

    analystmunge@yahoo.com

     
  • Date: Sun Sep 02, 11:45:00 PM EAT, Anonymous Mliakuvana

    Kawaida wilaya zote zina bustani za miche ya miti. Sina uhakika kama kuna miti/mimea asilia ila kuna miche ya miti mingi tu ambayo ni "native" ya maeneo hayo ingawa kwa kweli mingi ni ya mbao (pine, cypress) ya hedges (hekya(sp)) na ya makenchi, pulp and paper processing na kuni (eucalyptus) ingawa hii inapingwa sana siku hizi kwani inakunywa sana ground water, in the tune of debe 20 kwa siku, they say.

    Kwa wilaya ya Mufindi moja ya bustani ya miche Mafinga ipo kule Makalala karibu na makatekista na ile Mafinga au Don Bosco seminary(ya Changarawe). Bwana miti ni jamaa mmoja anajulikana zaidi kwa nickname yake ya "Mnoge" - alikuwa bonge ya full back 2 enzi zake timu ya Boma, na yeye husalimia kila mtu kwa neno hilo, mnoge?

    Bustani hizi zipo nyingi tuu all over Iringa I beleive. A good place to start, I think. The whole of Iringa vijijini, mjini, Kilolo, and huko Dabaga hakutakosekana miche ambayo ipo tayari kwa msimu huu wa mvua unaokuja.

    Ili miti iote haraka shimo lake liwe kubwa la kutosha debe liingie au ndoo ya Sadolin ya lita 20. Ukichimba na kuweka samadi mapema ili "ipoe" inakuwa bora zaidi. Shimo kama hili ni safi kwani linatoa ile top crust to get to the "good soil' below the top crust.

    Naomba kuwakilisha hoja.......

     
  • Date: Mon Sep 03, 03:12:00 PM EAT, Anonymous ANALYST

    Wanakijiji,

    Naomba niseme hivi,
    Tuna bahati ya kuwa na mwenyekiti anayependa kwenda vijijini, anayeleta habari za watu marginalised na kwa kweli yuko karibu na wananchi wa kawaida kabisa.

    Tumpe mandate.Ashirikiane na uongozi wa Mkoa na wilaya kuitisha kikao cha wenyeji. Baada ya hapo atuambie bila kuedit chochote "bila kupiga pasi" wananchi wanasemeaje. Mbona watu hawasiti kitisha vikao kuhusu UKIMWI si kwa kuwa ni janga? Uharibifu wa mazingira sii janga pia? Tutumie mbinu za kisasa kabisa kupambana na tatizo siyo kurudia yale yale kila mwaka yaani kampeni na zima moto!

    Hapa tunaweza kugeuza kijiji kuwa library ya indigenous knowledge ya makabila ya Iringa. Tuweke kumbukumbu hata picha za wazee vikongwe na wosia wao juu ya mstakabali wa Mkoa wetu. Je wanatushauri vipi? Je watakuwa tayari kunusuru mazingira? Nini kifanyike? Wana grudges gani ambazo in a way zina wafanya waone mazingira hayawahusu? I know wasomi wataona hili halina msingi maana hata kwenye mtandao unaweza kusoma kuhusu tree planting etc lakini huku ni kulikosea heshima bara la Afrika.

    We need to go back to square one, kama uelewa wa kisayansi tunao tayari basi tujiweke karibu na wanachi wasione tuna waburuza na ma degree na madiploma yetu. Lets share the knowledge for sustainable development.

    Tuanze na kaeneo kadogo tu na wanakijiji wachache kabisa, kijiji kimoja kinatosha kama pilot project. ujenge ukaribu kiasi kwamba watu wataona kama ni kazi ya ukoo kwenda kunyweshea miti mvua zinapo kosekana. Siyo kazi za serikali au chama cha mapinduzi.


    Tuchakue eneo ambalo ni manageable kwa ukubwa. Tisifanye zimamoto ya kutaka kuubadili mkoa mzima wa Iringa kwa msimu mmoja. That wont work. Regenerating nature requires patience and commitment. Sometimes only grandsons and daughters live to enjoy the full benefit.

    Nawasilisha

    analystmunge@yahoo.com

     
   
 
Copyright 2006 © MAGGID MJENGWA. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu