GAZETI LA UCHAMBUZI MAKINI LENYE KUIHUSU NA KUIGUSA JAMII. NI GAZETI LA KILA WIKI. LITAANZA KUONEKANA MITAANI JUMANNE, MACHI 31, 2009. USIKOSE NAKALA YAKO!
Saturday, October 28, 2006
Hii Ndio Mwananyamala. Inatisha!
Mazingira yanatisha. Mtoto aliyeshika tairi anakua akiizoea hali ya uchafu huu. Nyuma yake kuna watoto wenzake wanaocheza karibu na mfereji wa maji machafu. Nyuma kushoto kuna kijiwe cha vijana. Hawana ajira. Katika mazingira haya kipindupindu na malaria vitaendelea kuua watoto wetu na hata watu wazima. Hivi hizi pesa za MKUKUTA zinatumika vipi? Na wasomi wetu wanaijua hali hii halisi. Kwanini tunafumbia macho?
 
©Maggid | Date:28.10.06 | Permalink| | Send To Your Friend |


Comment: 9


  • Date: Sat Oct 28, 10:59:00 PM EAT, Blogger Jeff Msangi

    Maggid,
    Nimeiangalia picha hii kwa takribani dakika kumi nzima bila kupekua kope.Nimeitolea macho namna hiyo sio kwa sababu siamini bali imenikumbusha hali halisi ya mazingira mengi nchini Tanzania,sio Mwananyamala peke yake.
    Pamoja na hayo swali moja la msingi sana sina budi kujiuliza,hivi ni jukumu la nani kusafisha mazingira? Katika nchi kama hii ninayoishi ni jukumu la serikali za mitaa,jiji nk.Lakini tofauti moja kubwa hapa ni kwamba serikali hizi za mitaa,jiji nk zinawezeshwa na kodi za wananchi.Hali najua ni tofauti nchini mwetu.Utaratibu wa kulipa kodi bado haupo na sababu ni kwamba wananchi hawaamini katika kazi ya kodi zaidi ya kwenda kujaza matumbo ya "waheshimiwa".Sasa basi hapo nadhani jukumu la kusafisha mazingira yetu linarudi kwa mwananchi mwenyewe.Sikubaliani na kisingizio cha umasikini kama matokeo ya uchafu uliokithiri namna hii.Unaweza kuwa na nguo iliyochoka lakini hiyo sio sababu ya kutoifua na kuipiga pasi.
    Kinachotokea hapa ni kwamba viongozi wa mitaa,wale wajumbe na mabalozi wa nyumba kumi kumi(hivi bado wapo?) hawajui kazi zao.Mabwana na mabibi afya wa huko wanatakiwa kufukuzwa kazi mara moja.Pia umuhimu wa kujitolea haupo kabisa inaonekana! Kwanini?

     
  • Date: Sun Oct 29, 08:00:00 AM EAT, Blogger luihamu

    Kaka Majjid,hao vijana kwanini wasichukuwe jukumu la kusafisha mazingira au wanasubiri umoja wa mataifa?Kwa mtazamo wangu wengi tunapenda kufanyiwa mambo,kwa lugha nyingine tunategeana.Sio jukumu la serikali ni jukumu letu sisi wananchi kuisaidia serikali.Sasa hao vijana wanaketi na kupiga gumzo siku nzima hata kuchukwa fagio na kufagia wanaona noma.Inabidi tubadilike.

     
  • Date: Sun Oct 29, 12:49:00 PM EAT, Blogger rhxoqsa

    Hili ni kosa kubwa sana kumwaga maji machafu barabarani, mwenyekiti wa mtaa na Bw/Bi Afya lazima awajibike, mimi nakaa uswahilini Ilala na Bibi Afya wetu huku ni mnoko kweli kweli yaani hata ukifua na kumwaga maji barabarani basi ujue unalo akikushika, pia wana utaratibu wa kukagua mazingira ya nyumba kuanzia maua miti na mifugo na anahakikisha mbwa wote wamechanjwa na anakagua vyeti na hakuna mazalio ya mbu wala vichaka, huwa napata tabu sana kwenye baadhi ya nyumba ila huwa anakomaa nao, nilisahau pia huwa anahakikisha vyombo vya taka vyote vina mifuniko

     
  • Date: Sun Oct 29, 12:59:00 PM EAT, Anonymous Joel

    Jamii za kiafrika husasan bongo zina kazi kubwa mbele yake ya kubadilika kimawazo,kimila,kiutamaduni n.k. ili nazo ziendelee[cultural revolution]!Nyumba yako inapovuja anayeumia nani?Badala ya kulalamika na kungojea misaada inabidi kuchakarika mwenyewe kuikarabati au mpaka upigwe bakora,utishwe,ubembelezwe n.k.Hivi hapo akitokea mtu akaanza kufanya usafi si ajabu wakamzomea na kumuona fala badala ya nao kujiunga naye!Kuna wakati nilikuwa nikirudi bongo likizo basi nilikuwa nachukua kwanja langu kufanya usafi pale nyumbani basi wacha maneno ya maswahiba/majirani pale mtaani, hivi huyu mtu katoka safari majuu hapumziki nasi hapa kijiweni kutupa stori na ofa lukuki za moja moto moja baridi!Yeye kila kukicha anatupigia kelele na kwanja lake sijui ana mdudu gani kichwani?!Kwa mwendo huu washkaji kazi kubwa tunayo kuja kuwafikia wenzetu waliondelea!!!
    Joel.

     
  • Date: Sun Oct 29, 01:19:00 PM EAT, Anonymous Halifa Mjengwa

    Jamani haya mambo yanawezekana kufanyika. Wala haitajiki mtu wa mbali kusema. Tatizo hapa ni elimu na ufahamu wa mambo hakuna kingine. Serikali ni watu na watu wenyewe ndio hao wa mwanyamala, kota, mabibo, manzese, ilala na kwingineko. Kwa hiyo wao kama serikali wanawajibika kusimama na kufanya yale wanayoyataka kufanya. Kama wanaamua sasa ni mwanyamala yetu iwe safi basi itakuwa safi. Mji ninaokaa jana ilikuwa ni siku ya usafi wa eneo letu sisi wenyewe wananchi wa eneo hili ninalokaa tumefanya usafi wa jumla yaani kuzunguka nyumba zetu na maeneo ya michezo ya watoto wetu. Na sehemu ya kodi zetu ambazo tunalipa kama wananchi inarudi kwetu kama malipo na sio kwa wote ni kwa wale tu wanaoshughulika au watakaoshiriki katika usafi. Ni sio malipo makubwa ni chakula cha mchana tu, nia sio kulipana bali kupeana motisha na wala sio pesa bali ni chakula baada ya usafi tunakula pamoja chakula ambacho kinalipiwa na manispaa ya mji. Sasa haya kama yanawezekana huku kwanini yasiwezekane mwanyamala, kipawa, kiwalani, vingunguti? Hawa wanatakiwa kuamshwa kwamba Tanzania ni ya kwao na serikali ni wao na sio Kikwete peke yake kwa hiyo wana haki ya kufaidi matunda yao na kama wanawawakilisha wanashindwa kuwapa matunda ya michango yao basi wana haki ya kudai na ikibidi kuchukua kwa nguvu kilicho chao. Hii sio elimu ya kurusha roketi angani na wala sio elimu ya kutengeneza tochi, wala huitaji kumaliza darasa la saba kujua haya yote, ni swala la muda mfupi wa watu kusema Ya Basta (sasa basi). Kama Zapatistas (Mexico), Cochabamba (Bolivia), Sputh Africa na kwingineko walisema Ya Basta kwa nini Mwanyamala wasiseme?!!!!!!

    "Adui yako mwombee njaa na mnyime Elimu" By Halifa Mjengwa

     
  • Date: Mon Oct 30, 07:34:00 PM EAT, Blogger Maggid Mjengwa

    Jeff, Luihamu, hxhoqsa, Joel na Halifa,
    Kwanza nawashukuru sana kwa kushiriki kuchangia maoni yenu na juu ya nini kifanyike kule Mwananyamala na kwingineko. Hakika hoja zenu zilibeba maswali mengi pia. Kwa vile bado niko Dar, jioni ya leo nikaona ni heri nifanye ziara ya miguu pale pale Mwanyamala Bwawani ili nipate majibu ya maswali yenu. Maswali yenu yamenisaidia kuwa na mazungumzo mazuri na Balozi wa nyumba kumi Mama Sabrina na baadhi ya wakazi akiwamo mama Zawadi. Kwanza walifurahi sana na kufarijika kusikia kuna Watanzania wako ughaibuni wenye kuwajali na kujadili matatizo yao. Hakika nimepewa picha nzima ya tatizo na kuelimika zaidi. Kuna mmojawenu amesema kuna umuhimu wa wananchi kuisaidia serikali. Lakini pale Mwananyamala Bwawani Mama Zawadi amewauliza, watafanyaje pale Serikali inapokataa kusaidiwa? Wao tatizo wanalijua, wako tayari kushiriki kulitatua. Mathalan mfereji ule mkubwa wa maji unaonekana pichani hautoki. Umeishia njiani kwa vile pale ulipotakiwa kupita na kuendelea kwenye mfereji mkubwa kuna nyumba ya Mheshimiwa Diwani!
    Hakika hali yao ni ngumu na sasa wanasema ni afadhali kwa vile jua ni kali. Mvua zikianza mahala hapo panatisha zaidi. Mbu ni wengi hata sasa na malaria kwa watoto ni shida kubwa. Wakazi wale waliniruhusu kupiga picha zaidi ambazo mtaziona katika siku mbili tatu zijazo.

     
  • Date: Tue Oct 31, 06:25:00 PM EAT, Anonymous Madakomulume

    Jeff nakubaliana na wewe kuwa kazi ya kusafisha hapo ni ya serikali na wala sio eti watu wajitolee. Kuokota mifuko ya rambo kila siku hakuwezi kufanya sehemu hiyo iwe safi maana mambo yatajirudia tu na hatimaye watu watachoka. Cha muhimu ni miundo mbinu ya uhakika.
    Ila Jeff sikubaliana na wewe kuwa watu hawalipi kodi, hata wewe huko unakoishi sidhani kama unafuatwa na kuambiwa toa kodi, bali ukienda dukani kununua soda, shirt, chumvi, maharage ndipo unakutana na kodi huko. Hata hapa kwetu basi kwa mtindo huo tunalipa kodi kwa sana bila shaka umeshawahi kukisikia kitu kikiitwa VAT, tunalipia hadi viberiti, koroboi ya mafuta ya kupikia, mkate n.k suala nikuwa wajanja wachache wanatafuna mishiko hiyo.
    Umefika wakati wananchi waelezwa huduma nzuri ni haki yao na siyo upendeleo kwani kodi wanalipa!

     
  • Date: Tue Oct 31, 09:33:00 PM EAT, Anonymous HH

    Mimi nadhani swala la usafi au uchafu linaanzia kichwani kwa kila mtu, hivyo kama kweli hawa wakazi wangekuwa wanapenda mazingira yao yawe safi kuna kitu wangefanya kuonyesha wanakerwa na uchafu hata huyo Diwani aliyejenga na ku-block huo mtaro angeonja joto ya jiwe. Ttatizo letu wa-Tanzania ni kutokuwa tayari kupigania haki zetu, kila mtu anataka fulani afanye mwisho kila mtu anaacha baadae tunazoea na kuona ni kitu cha kawaida. Maggid huyo Mama Zawadi na wenzake baada ya kuona mfereji unaishia kwenye nyumba ya diwani wamechukua hatua gani au ndio diwani yuko juu ya sheria ya serikali za mitaa. Mimi nadhani hawa wakazi wanapenda uchafu ndio maana kila mtu ame-relax. Niliwahi kutembelea Japan nikatembezwa sehemu mbalimbali na mwenyeji wangu, moja ya sehemu hizo ilikuwa shule ya watoto (shule ya vidudu) usafi na mandhariya shule yalinivutia sana nilifanikiwa kuongea na mwalimu mmoja akaniambia wao wanasisitiza usafi kuliko kitu kingine chochote especially kwa watoto wadogo - hivyo watoto wanakua wakichukia uchafu na kupenda mandhari safi - samaki mkunje angali mbichi - je sisi tunatoa uzito gani kwenye elimu ya usafi na mazingira? kiasi kwamba watoto wakirudi majumbani wawe changamoto kwa wazazi kuweka mazingira safi?

     
  • Date: Tue Oct 31, 11:03:00 PM EAT, Blogger Maggid Mjengwa

    HH:
    Hoja zako nimezikubali na maswali yako ni ya msingi. Hakika baadhi ya unayojiuliza niliwauliza wananchi wale, lakini wanaonekana kukata tamaa mno. Halafu hilo la kuprotest haliko katika fikra zao ingawa ingekuwa njia mojawapo ya kupata suluhu ya matatizo yao.

     
   
 
Copyright 2006 © MAGGID MJENGWA. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu